Menu
in , , ,

Trapattoni, Domenech waitaka Ivory Coast

*Mliberia atia nia kugombea urais Fifa

Makocha 59, wakiwamo wakongwe Giovanni Trapattoni wa Italia, Raymond Domenech wa Ufaransa na Mwingereza Dave Jones wametuma maombi ya kuchukua nafasi ya ukocha wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast.

Trapattoni amepata kuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Ireland, Domenech aliwafundisha Ufaransa wakati Jones alikuwa bosi wa klabu ya Sheffield Wednesday.

Wote hawa wapo kwenye mkururo wa kutaka kumrithi kocha wa Les Elephants (Tembo) kwa ajili ya kumrithi kocha aliyewaletea ubingwa wa Afrika, Herve Renard.

Shirikisho la Soka la Ivory Coast (IFF) lipo kwenye mchakato wa kupata kocha ili kupeperusha vyema bendera ya taifa hilo, ambapo litafanya mchujo hadi makocha watatu watakaofanyiwa usaili kupata mmoja.
IFF imechapisha majina ya makocha wote walioomba kazi hiyo, katika kile inachosema kwamba ni uwazi. Pamoja na wakongwe hao, mwingine aliyeomba nafasi hiyo ni kocha wa sasa wa Nigeria, Stephen Keshi, ambaye katika hali ya kushangaza alisaini mkataba na Nigeria Aprili hii tu.

“Jina la kocha ajaye wa Tembo atajulikana mwishoni mwa Juni au mwanzoni mwa Julai,” taarifa ya IFF imesema baada ya kuorodhesha majina hayo.

Jones aliyefukuzwa Sheffield Wednesday 2013 ndiye Mwingereza pekee kwenye orodha hiyo ndefu yenye Wafaransa 17 na pia wengine 17 kutoka Italia. Wafaransa ndio waliowatawala Ivory Coast.

Mwingine ni kocha wa zamani aliyefukuzwa Gibraltar, Allen Bula pamoja na Mreno Paulo Jorge Silva asiyekuwa na uzoefu wa kimataifa.
Domenech na Trapattoni wamepata kufundisha timu zilizotinga fainali za Kombe la Dunia mara kadhaa na ndio wanaopewa nafasi kubwa zaidi ya kuchukua nafasi hiyo.

Mwaka mmoja uliopita ulishuhudia Trapattoni akidai kwamba alikuwa karibu kupata kazi ya kuwafundisha Ivory Coast lakini Renard akatwaa kazi hiyo.

Iwe iwavyo, atakayechukua nafasi hiyo atakuwa na kazi ngumu ya kurejesha mafanikio aliyofikisha Renard aliyehamia Lille ya Ufaransa.
Rais Alassane Ouatarra aliwazawadia wachezaji na viongozi wa Ivory Coast nyumba na fedha nyingi baada ya kutwaa ubingwa.

BILITY WA LIBERIA ATAKA URAIS FIFA

Liberia Football Association president Musa Bility has confirmed he will stand for the presidency of FIFA
Rais wa Shirikisho la soka la Liberia (LFA) Musa Bility amethibitisha kuingia katika mbio za kuwa boss wa FIFA

Mwenyekiti wa Chama cha Soka (FA) cha Liberia, Musa Bility ametangaza nia yake ya kugombea urais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), akisema kwamba hii ni zamu ya Afrika kushika uongozi.

Bility (48) anakuwa mtu wa pili kutangaza nia ya kugombea urais baada ya Zico wa Brazil asiyekuwa na uzoefu wa nafasi za uongozi kwenye soka.

Uchaguzi unatarajiwa kufanyika baada ya miezi kadhaa kwani Rais Sepp Blatter ambaye uongozi wake wa muda mrefu unashutumiwa kwa rushwa, wizi na utakatishaji fedha anatarajiwa kujiuzulu.

“Afrika wana eneo kubwa zaidi la upigaji kura katika Fifa na lazima tuchukue uongozi ili kuwaleta watu wa soka pamoja. Tunakubaliana sote kwamba soka ipo kwenye wakati mgumu na ndipo viongozi mahiri wanapochipukia,” anasema Bility.

Mliberia huyo ameongoza FA tangu 2010 ambapo Rais wa Shirikisho la Soka la Afrika (Caf), Issa Hayatou alibwagwa na Blatter kwenye uchaguzi wa 2002.

Bility anataka mazonge ya sasa ya Fifa kushughulikiwa kwa uwazi, uboreshaji wa jinsi masuala ya fedha yanavyosimamiwa lakini pia maeneo masikini zaidi yasaidiwe kwenye ukuzaji soka.

Bility pia angependa kuona madaraka makubwa yaliyo miongoni mwa wajumbe 24 wa Kamati ya Utendaji ya Fifa yapunguzwe.

Ameahidi kuanzisha ushirikiano mkubwa baina ya Fifa na Interpol kwa ajili ya kufanikisha uchunguzi na hatua za kisheria dhidi ya wanaojihusisha kwenye vitendo vya jina chini ya mwavuli wa Fifa au kutumia rasilimali za shirikisho hilo.

Mwezi uliopita, mamlaka ya Marekani yaliwashitaki viongozi saba wa Fifa na wengine saba nje ya shirikisho hilo kwa makosa ya kujihusisha na mlungula.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Exit mobile version