*Tegemeo la kuwabakisha Liverpool juu
HATIMAYE Liverpool wameongeza mchezaji muhimu mno, na huenda akaonesha tofauti kubwa na wengine kwenye timu za Ligi Kuu ya England (EPL).
Huyu ni kiungo mahiri kutoka Hispania na mtaalamu wa pasi, Thiago Alcantara ambaye kuna kila dalili kwamba atawahakikishia Liverpool kubaki matawi ya juu, wakiwa ni mabingwa watetezi.
Kocha Jurgen Klopp aliamua kumnunua mchezaji huyo ikiwa ni njia ya kuongeza soka yao ya kupambana kwa kutia shinikizo na kuwakandamiza wapinzani wao kwa kasi. Alionesha kwanza umahiri wake kwenye mechi ya kwanza baina ya Liverpool na Chelsea, ambapo Klopp alimzamisha Frank Lampard.
Liverpool walipotwaa ubingwa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL), ilionekana wazi kwamba walikuwa wakali sana, lakini kuwa bado kulikuwa na kitu kinasubiriwa, na wakadhihirisha hilo kwa kutwaa ubingwa wa UCL.
Hata hivyo, wakielekea kuvikwa taji hilo la pili, walipoteza ubingwa wa Ulaya lakini pia wakafungwa kwenye mechi kadhaa za EPL, wakati wakiwa wanatafuta kuishika rekodi inayoshikiliwa na Arsenal pekee ya kutopoteza hata mechi moja kwenye msimu mzima, enzi za Invicibles.
Liver wamechukua ubingwa ikiwa ni miaka mitano tangu Klopp kujiunga nao, akiijenga timu taratibu na kuiimarisha. Ilikuwa pia ni miaka 30 ya kusubiri tangu walipotwaa ubingwa huo kwa mara ya mwisho. Baada ya kuonesha kuchoka, hasa wakiwa wamepumzika kifupi baada ya kumalizika msimu, walipaswa kujiimarisha, na huko ni sawa kwa kumpata mtu wa aina ya Alcantara.
Huyu atawasaidia kupambana na maadui wao wakubwa – Manchester United, Manchester City, Chelsea, Arsenal na wengine wasiotabirika. Liver waliwavua ubingwa Liverpool. Alcantara ni kiungo mahiri wa kati aliyezaliwa miaka 29 iliyopita na yumo kwenye Timu ya Taifa ya Hispania – La Furia Roja.
Alizaliwa nchini Italia, akiwa motto mkubwa wa mchezaji wa zamani Manzinho na alijiunga na Barcelona akiwa na umri wa miaka 14, akaanza rasmi soka ya ushindani 2009. Ameshinda makombe kadhaa akiwa na Barca ikiwa ni pamoja na ubingwa wa Hispania na Ulaya na hata Kombe la Dunia kwa taifa lake kabla ya kujiunga na Bayern Munich 2013. Akiwa Ujerumani amejikusanyia makombe 16, na sasa anataka ya England.