Menu
in , , ,

TFF/TWFA kusheheresha Siku ya wanawake Duniani

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania kwa kupitia kamati ya wanawake na chama cha mpira wa miguu kwa wanawake wanatambua umuhimu wa siku ya wanawake duniani.Mpira wa miguu kwa wanawake ni moja ya michezo inayokuwa kwa kasi katika bara la Afrika na hata hapa nyumbani.Idadi ya wasichana wanoshiriki katika mpira wa miguu imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.

Katika kusheherekea siku ya wanawake duniani mwaka 2014. Sherehe rasmi zitafanyika katika mkoa wa Tanga

TFF /TWFA wanaamini kuwa ili kuwa na kiwango kizuri na maendeleo katika mpira wa miguu wanawake ni lazima kuanza na vijana wadogo hivyo basi Shirikisho na chama cha mpira wa miguu Tanga limeandaa mafunzo kwa walimu wapatao 30 toka shule15 za mkoa wa Tanga.

Walimu hao watapatiwa mafunzo kwa siku mbili na tarehe 08/03/2014 kutakuwa na Tamasha la Grassroot litakalojumusha jumla ya wanafunzi wapatao 1000 toka shule husika.

Ni matumaini ya shirikisho kuwa mafunzo hayo na tamasha la grassroot litaleta mwamko wa mpira wa miguu katika mkoa wa Tanga na hamasa kwa watoto wa kike,wasichana na kina mama katika ushiriki wa mpira wa miguu wanawake

51.556643-0.117687

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version