Shirikisho la soka hapa nchini (TFF) linaendelea na harakati zake za kuanzisha soka la ufukweni hapa nchini baada ya kupewa mamlaka hayo na shirikisho la soka Dunia (FIFA)
Katibu mkuu wa TFF Fredrick Mwakalebela amesema hivi sasa kila kitu kinaenda vizuri na tayari baadhi ya watu wameshajitokeza kwa TFF kwa nia ya kuanzisha vilabu vya mchezo huo
Pia katibu huyo anasema kwa kuanzia wao TFF wameona kwanza mchezo huo uanze hapa jijini Dar es salaam kwa majaribio na baadae ndio uende kwenye mikoa mingine ya Pwani kabla ya kuenea kwenye mikoa mingine ya Tanzania
Hivi sasa kuna baadhi ya vilabu vichache ambavyo havipo rasmi vinacheza soka la ufukweni hapa jijini Dar es salaam na TFF ndio linazungumza na vilabu hivyo ili kuona kama wanaweza kuanzia huko
Mwakalebela amesema ili kuweza kuvitambua vilabu hivyo ameomba vijisaili kwa TFF ili viweze kutambulika na kama watafanikiwa basi wanaweza kuanza kuanda mashindano hayo kwa kuanzia kwa vilabu hivyo vichache
Mwisho kabisa Mwakalebela amesema FIFA wamekubali kutoa mafunzo ya kuendesha soka hiyo hapa nchini na ndiomana wameviomba vilabu hivyo kufanya usajili haraka ili waweze kupata mafunzo hayo toka FIFA