Baada ya hapo jana Rais wa chama cha soka cha Kenya (Kenya Football) Mohamed Hatamy kusema wapo tayari kushirikiana na Tanzania kuanda michuano ya mataifa ya Africa ya mwaka 2016 hii leo jumatano shirikisho la soka hapa nchini Tnzania (TFF) limesema nalo lipo tayari kufanya hivyo.
Katibu mkuu wa TFF Fredrick Mwakalebela amesema swala hilo ni la kisera zaidi na wenye uamuzi wa kutoa kauli ya mwisho ni kamati ya utendaji ya TFF.
Mwakalebela anasema kama swala hilo likija rasmi kwenye ofisi yake basi litafikishwa kwenye kamati hiyo ili liweze kujadiliwa na anahakika halitapingwa hata kidogo.
Pamoja na yote TFF imesema hadi sasa bado haijapata ombi rasmi toka kwa Kenya Football kuhusu swala hilo bali wanalisikia kwenye vyombo vya habari tu lakini wao hawana shida wakati wowote ule likatapokuja watalipokea kwa mikono miwili na kulijadili.
Kamati ya utendaji ya TFF itakutana mwezi ujao kwenye ukutano wake wa kawaida na kama swala hilo litawafikia haraka kabla ya mkutano huo basi litapekwa ili liweze kujadiliwa.
Wakati huohuo kamati ya ufundi ya shirikisho la soka hapa nchini (TFF) limepitisha majina ya makocha wawili toka nchini Brazil kuja hapa nchini kufundisha soka.
Makocha hao mmoja ni kocha wa timu ya taifa za Vijana wa chini ya miaka 21 na chini ya miaka 17 na mmoja ni kocha wa viungo na hivi karibuni majina yao yatawekwa hadharani.
Ikumbukwe majina ya makocha hao yaliletwa na kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Marcio Maximo alipoenda nyumbani kwao Brazil kwa mapumziko.
Hivi sasa timu za taifa za soka za vijana za Tanzania hazina kocha baada ya aliekuwa kocha wa timu hizo Marcus Tinoco toka Brazil kuondoka baada ya kupata kazi kwingine na kumaliza mkataba wake .