Menu
in , , ,

TETESI ZA USAJILI -Charles Hilary Asajili rasmi…..

TETESI ZA USAJILI
Sterling ameleta shida
*Yaya Toure, Oscar, Pelle watakiwa Italia
*Pogba Chelsea? Hummels huenda Man U
Wakati Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers akiapa kwamba mshambuliaji wao, Raheem Sterling haendi popote, Chelsea wameingilia kati.
Sterling amekataa ofa ya mkataba mpya na mshahara wa pauni 100,000 kwa mwezi Liverpool, akisema wangefanya hivyo kiangazi kilichopita angekubali.
Arsenal kuona hivyo wakaingia kwa nguvu na wapo tayari kumwongezea Sterling mshahara ili ahamie kwao kiangazi hiki, lakini Rodgers anakataa kama alivyofanya kwa Luis Suarez.
Wakongwe wa soka wa England, wakiwamo wachezaji wa zamani wa Liverpool wameonya kwamba Sterling (20) bado ni mdogo na hajafikia sifa za wachezaji mahiri duniani, hivyo shinikizo sasa lipo kwake.
Chelsea wamesema kwamba kwa hali ilivyo Anfield nao wanafikiria kuingiza ‘majeshi’ yao ili wamnase kinda huyo mwenye asili ya Jamaica.
Yote haya yanakuja wakati Liverpool wakiwa katika mbio za kuwania walau nafasi ya nne katika Ligi Kuu ya England (EPL), wakishika nafasi ya tano wakiwa na pointi 54.
Mbele yao wapo Manchester United wenye alama 59, Arsenal alama 60, Manchester City alama 61 na Chelsea alama 67.
Wikiendi hii wanacheza na Arsenal dimbani Emirates na pengine washabiki wa timu zote mbili watamtolea macho Sterling.
NYOTA WENGINE NA MAMBO YAO
Mlinzi wa Borussia Dortmund, Mats Hummels (26) ameendeleza utata juu ya hatima yake, kwani amedaiwa kuwaambia wachezaji wenzake wa Ujerumani kwamba anakaribia kutimkia Manchester United.
Wana Old Trafford pia wapo tayari kutoa pauni milioni 11 kumpata mlinzi wa Lille na Denmark, Simon Kjaer (26).
Juventus wa Italia wanafikiria kutoa ofa kwa Chelsea ili wawauzie kiungo wao Mbrazili, Oscar (23). Tayari Kocha Massimiliano Allegri amewaambia wamiliki wafanyie kazi suala hilo.
Wataliano wanaonekana kuja juu, kwani Inter Milan wanataka kumsajili kiungo mahiri wa Manchester City na Ivory Coast, Yaya Toure (31)
Ama kwa upande wa Manchester United, Kocha Louis van Gaal anadaiwa kwamba mchezaji anayempa kipaumbele kujiunga nao kiangazi hiki ni kiungo wa Uholanzi, Kevin Strootman (25) anayecheza Roma.
Inaelezwa kwamba amesema hana haja ya kumrejesha United mchezaji wao wa zamani, Paul Pogba anayetafutwa na Chelsea.
Ilivyo ni kwamba, Chelsea wapo tayari kuwauza viungo Oscar au Ramires katika sehemu ya dili hilo. Wakimkosa Pogba, watamfuata kiungo wa  Atletico Madrid, Koke (23).
Klabu nane zinapigana vikumbo kumsajili mshambuliaji wa Liverpool aliyeshindwa kuchanua Anfield, Fabio Borini (24).
Lazio wa Italia wameanza kumfuatia Mtaliano anayekipiga Southampton kama mshambuliaji, Graziano Pelle (29) ili kuchukua nafasi ya Miroslav Klose (36) anayetarajia kustaafu kiangazi hiki.
Kicha wa Crystal Palace, Alan Pardew anatarajia kusajili wachezaji wanne baada ya klabu hiyo kutengeneza faida ya pauni miloni 23.
Naye bosi wa Everton, Roberto Martinez anasema hana wasiwasi na Romelu Lukaku kubadili wakala, wala kwamba atahama klabu hiyo karibuni.
Kocha wa Swansea City, Garry Monk anasema kwamba kipa Lukasz Fabianski (29) atabaki klabuni hapo licha ya kutakiwa na Roma.
Nahodha wa zamani wa Liverpool, Phil Thompson amesema Liver wanatakiwa kusajili mshambuliaji mwingine.
Anawataja wanaofaa kuwa ni wale wa Paris St-Germain, Ezequiel Lavezzi (29) au Edinson Cavani (28) na kama vipi wamchukue mpachika mabao wa Napoli aliyetoka Real Madrid, Gonzalo Higuain (27).

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version