Menu
in , , , ,

Terry achafua hali ya hewa

*Agomea mkono wa mwenyekiti FA

 

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya England, John Terry amechafua hali ya hewa kwa kukataa mkono wa bosi wa FA.
Terry ambaye pia ni nahodha wa Chelsea, alikataa mkono wa Mwenyekiti wa FA, David Bernstein wakati wa hafla ya kurudisha kombe la Ubingwa wa Ulaya.
Terry alikiri kwa macho makavu kwamba alikataa kupokea mkono wa Bernstein, lakini mwenyekiti huyo alidai hakumaizi hilo, ila akasema ni upuuzi mtupu.
Hilo lilikuwa tukio kubwa kimataifa kwa soka, kwani wakuu wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) walikuwapo, akiwamo bosi wao, Michel Platini, ambapo timu yenye kombe hulikabidhi.
Chelsea walitwaa kombe hilo mwaka jana, na wakavunja rekodi vibaya kwa kuwa timu ya kwanza kushindwa kuvuka hatua ya makundi katika mashindano yaliyofuata.
Mbaya zaidi ni kwamba fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka huu zinafanyika katika Uwanja wa Wembley.
Timu nne zilizofuzu hatua ya nusu fainali ni Barcelona, Bayern Munich, Borussia Dortmund na Real Madrid, jozi za kwanza zikichuana kama ilivyo kwa jozi za pili.
Terry atakuwa amekasirishwa na uamuzi wa mwisho wa Bernstein wa kumvua unahodha wa England baada ya mchezaji huyo kuwa ameshitakiwa kwa kumkashifu kibaguzi mweusi Antony Ferdinand wa QPR.
Uamuzi huo ulisababisha aliyekuwa kocha wa England, Fabio Capello kujiuzulu, ambapo licha ya mahakama kumsafisha Terry katika hoja zilizozidisha utata, FA ilimtia hatiani na kumpa adhabu.
Terry alifungiwa mechi nne na £220,000, jambo lililomchukiza na kuamua kuachana na timu ya taifa. Hata hivyo wadau wengi walichukulia kwamba adhabu hiyo haikuwa kubwa vya kutosha.
Alipoulizwa Ijumaa kwa nini hakupokea mkono wa mwenyekiti, Terry alisema: “Sikiliza, hili ni jambo gumu kwangu. Ni wazi ndiye aliyesimama kunikandamiza kwenye ile kesi mahakamani, akasema vitu nisivyotaka kusema hewani, nadhani ni suala tunalotakiwa kuepuka tu.”
Mwenyekiti wa FA, Bernstein ambaye amebakisha miezi michache aondoke madarakani, alisema haya kuhusu suala lake na Terry hiyo jana:
“Sikumaizi chochote, uhusiano wangu na kila mmoja hapa ni mzuri…nadhani tuzungumzie mambo chanya zaidi kuliko upuuzi.
Alipobanwa kuhusu uhusiano wake na Terry, Bernstein alisema wapo mbali mbali kidogo, lakini akasema si jambo linalomfikirisha, kwa sababu ana mengi ya vipaumbele kufanyia kazi kwa muda wake mfupi uliobaki.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version