Menu
in , , ,

Stephen Keshi bosi tena Nigeria

 

Nigeria wamemteua tena Stephen Keshi kunoa Timu ya Taifa ‘Super Eagles’ kwa mara nyingine na amesaini mkataba wa miaka miwili.

 

Keshi aliwaongoza Nigeria kutwaa ubingwa wa Afrika 2013 lakini mkataba wake haukuongezwa baada ya michuano ya Kombe la Dunia 2014.

 

Baada ya hapo alikuwa akifanya kazi kwa mtindo wa ‘deiwaka’, kwa maana kwamba alikuwa akilipwa kuendana na mechi alizosimamia na dili hilo linaisha baada ya kushindwa kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2015.

 

“Tunaanza upya. Tunahitaji kuungwa mkono na washabiki wetu, vyombo vya habari na kila Mnigeria arudi kwenye timu ambayo sote tunamilikiwa. Nikiwa kocha na mchezaji wa zamani niliumia sana kwa kushindwa kufuzu kwenye michuano iliyopita.

 

“Bado nina imani kwamba safari hii tutakwenda vizuri, tutajiandaa vyema na kutakuwa na mafanikio makubwa. Ili kufanikiwa lazima tukae pamoja, kwa sababu Nigeria ni yetu – hii si timu ya Keshi bali ni ya taifa letu ,” anasema Keshi.

 

Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) linaeleza kwamba Keshi (53)amewekewa malengo ambayo asipoyafikia mkataba wake utavunjwa. Kadhalika ametakiwa kusaini kuridhia kanuni za maadili na anatarajiwa kufanya kazi kwa karibu na Kamati ya Ufundi ya Chama cha Soka Nigeria (NFF).

 

Bosi wa NFF, Felix Anyansi-Agwu amesema kwamba wana imani kubwa kwamba Keshi atawapandisha chati sana Eagles. Keshi akiwa mchezaji alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Afrika 1994 lakini msaidizi wake wa muda mrefu, Daniel Amokachi ameondoka na nafasi yake kuchukuliwa na Salisu Yusuf.

 

Yusuf aliwaongoza Kano Pillars kuwa mabingwa wa Nigeria 2008, na amepata kufanya kazi kama msaidizi wa Kocha wa Timu ya Taifa ya Vijana (U-20) naya wakubwa Samson Siasia.

 

Akiwa kocha wa muda, Keshi alikuwa na kipindi kigumu 2014, ambapo alifukuzwa na NFF, kabla ya Rais Goodluck Jonathan kuingilia kati na kumrejesha kazini. Katika mechi mbili za mwisho akiwa na Eagles,

 

Keshi hakupokewa vyema na washabiki jijini Abuja na Akwa Ibom.

Kazi kubwa iliyo mbele yake sasa, wakati Nigeria pia wakiwa wamepata Rais mpya, Jenerali Muhamadu Buhari, ni kuivusha timu kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2017, ambapo wamepangwa kundi moja na Tanzania, Misri na Chad.

 

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version