Menu
in

Stars `full mzuka` kwa Morocco leo

Marouane ChamakhImage via Wikipedia

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Morocco na klabu ya Arsenal ya England, Marouane Chamakh (kushoto) akipokea maelekezo kutoka kwa mmoja wa maafisa wa Morocco wakati wa mazoezi ya timu hiyo ya taifa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.

Kocha wa timu ya Taifa Stars, Jan Poulsen amesema kuwa hana cha kuhofia leo wakati timu yake itakapowakabili Morocco, katika mechi ya kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika 2012, ambayo Rais Jakaya Kikwete atakuwa mgeni rasmi.
Mdenmark huyo aliyeiongoza Stars katika sare dhidi ya Algeria ugenini katika mechi yake ya kwanza ya kimashindano tangu alipochukua madaraka hayo, alisema jana kuwa vijana wake wameiva na kwamba wamejengwa kisaikolojia kuikabili timu hiyo inayoshika nafasi 95 katika viwango vya ubora wa soka duniani baada ya kuanguka kwa nafasi 12 mwezi huu. Tanzania ni ya 111.
Nahodha wa Stars, Shadrack Nsajigwa alisema kuwa wachezaji wenzake wanatambua umuhimu wa mchezo wa leo na pia wanatambua dhamana kubwa waliyonayo kwa Watanzania hivyo hawatakubali kupoteza mchezo huo kwenye uwanja wa nyumbani, licha ya kukabiliana na timu yenye nyota wakubwa kama Marouane Chamakh wa Arsenal, El Hadoaui wa Ajax na Yosseuf Hadj, ambaye ni mdogo wa nyota wa zamani Afrika, Mustapha Hadj.
Akizungumza na wachezaji wa Stars jana, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera aliwataka waonyeshe nidhamu kwenye mchezo wao wa leo pamoja na kupambana hadi jasho la mwisho kama walivyofanya kwenye mechi yao ya awali dhidi ya Algeria.
Bendera aliwataka wachezaji wa Stars kutoogopa majina makubwa ya wachezaji wa Morocco na badala yake wazingatie maelekezo ya mwalimu wao.
“Hakuna haja ya kuwaogopa Morocco kwa sababu wao watakuwa 11 uwanjani na ninyi pia mtakuwa 11, naamini kama mtafuata maelekezo ya mwalimu wenu tutafanya vizuri kesho (leo)”, alisema Bendera.
Aliwaeleza wachezaji kuwa serikali na Watanzania kwa ujumla wapo nyuma yao na hivyo wana jukumu kubwa la kuleta raha.
Alisema kuwa Rais Kikwete atakuwapo uwanjani kama mgeni rasmi lakini pia atakuwepo uwanjani hapo kama shabiki anayeisapoti Stars kwa nguvu zote.
Mechi hiyo inatarajiwa kuanza saa 10 jioni na itaonyeshwa moja kwa moja na Supersport.
CHANZO: NIPASHE

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version