Ni miongoni mwa vyama vichache nchini vinavyopata ruzuku ili kuendeleza michezo ya walemavu wa akili.
Special Olympics Tanzania kilianza rasmi mwaka 1968 na aliyekuwa mkurugenzi Ustawi Jamii Ndugu Madai Nyapule mara tu baada ya kurudi masomoni Marekani.
Chama hicho kilianzishwa kwa msukumo mkuu toka kwa Sargent Major Shriver na mkewe Mama Shriver kwenda kwa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mwalimu Julius Nyerere.
Sargent Shriver alikuwa mwanzilishi wa shirikisho hilo toka Marekani. Mkewe Shriver ni dada wa aliyewahi kuwa Rais wa Marekani John F Kennedy. Bila shaka wengi wanakumbuka uhusiano wa karibu kati ya Mwalimu Nyerere na familia ya John F Kennedy.
Kwa pamoja waliazimia kuanzishwa kwa chama hicho nchini ili kitoe fursa kwa watu wenye ulemavu wa akili.
Mzee Shriver ambaye pia ni mkwe wa mcheza sinema maarufu marekani Shwarznigger alifariki mapema mwaka jana .Hata hivyo ndoa ya Shwarsnigger na binti huyo wa Shriver nayo haikudumu baada ya kuachana mwishoni mwa mwaka jana kwa kashfa ya Shwarsnigger kuzaa na mtumishi wa ndani .
Hata hivyo mtalaka huyo na kaka yake ni watendaji wakuu wazuri wa chama hicho kimataifa.
Pamoja na kupata ruzuku yakutosha kupitia Chama cha Special Olympics Ireland bado chama hicho kinasusua katika programs zake nyingi katika kushirikisha wanamichezo wake.
Chama hicho kina bodi maalumu ilioteuliwa na mkurugenzi mtendaji Ndugu Frank Macha.
Ukweli bodi hiyo haina maamuzi yoyote mbele ya mkurugenzi mtendaji
Ndugu Macha aliwahi kuwa maneja wa uwanja wa taifa Dar Es Salaam.
Hapo awali aliazimwa na Special Olympics Tanzania lakini kwa vile amestaafu kazi serikalini hivi sasa ni mtendaji wa kudumu katika chama hicho cha walemavu SOT.
Pamoja na kupata ruzuku tosha bado chama hicho hakina mipango madhubuti kuendeleza michezo kwa walemavu wa akili nchini.
Chama hicho hutumia pesa nyingi kwa posho za safari na mishahara minono badala ya kutumia kuendeleza walemavu wa akili.
Hadi sasa program nyingi za mikoa hazifanyi kazi zake kutokana na ushirikiano duni wa mtendaji mkuu wa chama hicho.
Wataalamu wengi waliofundishwa kukiendesha chama hicho wengi wamejiengua au kufukuzwa na mtendaji huyo mkuu. Bahati mbaya zaidi chama hicho hakina mkutano mkuu wa wanachama wala uchaguzi wa viongozi wake hivyo kutobadili uongozi na haswa wa juu hadi hapo watakapo tangulia mbele ya haki.
Ni muda mrefu sasa chama hicho hakijaendesha mashindano ya taifa wala kuendesha program zingine kitaifa
Uhusiano wake na vyama vya mikoa ni mbaya kiasi kwamba linahitajika Baraza la Michezo nchini kuangalia upya mienendo ya chama hicho katika kushughulikia walemavu wa akili nchini.