Menu
in , , , ,

Siri za Arsenal Ligi ya Mabingwa

Tanzania Sports

LIGI ya Mabingwa inarejea tena baada ya kupisha ratiba ya mechi za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026. Ligi hiyo imefikia hatua ya robo fainali ambapo Arsenal wanatarajiwa kumkaribisha bingwa mtetezi, Real Madrid katika mchezo wa kwanza utakaofanyika kwenye dimba la Emirates hapa London. Mchezo huu una sura kadhaa ikiwemo kwa Real Madrid kutaka kulipa kisasi baada ya kuchapswa 1-0 mwaka 2006 kwenye Ligi ya Mabingwa. 

Wakati huo Arsenal ilikuwa chini ya kocha Arene Wenger huku safu ya ushambuliaji ikiongozwa na nahodha wao Thiery Henry. Kuelekea mchezo huo kulikuwa na gumzo kwa pande zote mbili; Arsenal imepoteza baadhi ya wachezaji wake muhimu baada ya kupata majeraha, hali kadhalik Real Madrid ilikuwa inasubiri uamuzi wa UEFA ambao walikuwa wakichunguza tuhuma za uvunjaji wa kanuni zilizofanywa na wachezaji Antonio Rudiger, Kylian Mbappe, Dani Ceballos, na Vinicius Junior. Hata hivyo UEFA imetoza faini wachezaji hao badala ya kuwafungia kwa mchezo mmoja. Kelekea pambano hili TANZANIASPORTS inakuletea mambo matatu ambayo kocha wa Arsenal Mikel Arteta anayazingatia zaidi ili kuibuka na ushindi kwenye mechi zote mbili.

Mechi kubwa kwao

Tanzania Sports

Katika mazungumzo yake na jarida la AS kueleka kwenye mchezo huo, kocha Mikel Arteta amebainisha kuwa huo ni mchezo mkubwa mno kwa wachezaji wake, yeye binafsi na benchi la ufundi. Alisema mwishoni mwa wiki wamecheza na Everton ambapo ni mchezo mgumu wa Ligi Kuu kisha kuelekeza akili na mbinu katika mchezo wao unaofuata dhidi ya Real Madrid kwani ni mkubwa zaidi msimu huu hasa kupambana na bingwa mtetezi. “Kuwaondoa Real Madrid kwenye hatua hii ni jambo muhimu sana, na ndilo ninaloamini linawezekana. Kushinda dhidi ya Real Madrid ni chachu ya mipango ya Arsenal katika ushindani, na huu ni mpango wangu pia kushindana kwenye mashindano makubwa.”

Mikel Arteta alirudi hapa London kaskazini mwaka 2019, kipindi hicho klabu ya Arsenal ilikuwa kwenye nyakati ngumu kwa kila eneo. Hawakuwa na ushindani kwenye Ligi Kuu England. Hawakuwa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, na wala uwezo  wao wa kupambani ubingwa haukuwa karibu yao. “Yalikuwa mazingira magumu, ni magumu kwa kila eneo la timu kuanzia ndani ya uwanja hadi taswira ya nje,” anasema Arteta. Kwa misimu mitano aliyokuwa Arsenal, ameshuhudia alikosa kombe la EPL dakika za mwisho dhidi ya waajiri wake wa zamani Manchester City mara mbili.

“Mpango wetu ni kushinda mechi zote na kushinda taji na medali na kisha kuedneleza ushindani maeneo mengine na kuongeza medali pia. Mpango huo una maana Arteta amejipanga vyema kupambana na Real Madrid ambayo ni bingwa mara 15 wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Tanzania Sports

Arsenal wamekuwa na nyakati ngumu kwa kuwapoteza wachezaji wake ambao wamekuwa majeruhi na  wengine wamerejea kikosini. Miongoni mwa majeruhi hao ni Martin Odegaard, Gabriel Magalhaes, Gabriel Jesus, Ben White, Bukayo Saka ambao ni muhimu kwenye kikosi chake lakini walipitia nyakati zilizomnoa kocha huyo kwani hakuonekana kuyumbishwa na hilo. Anasema Arsenal ni klabu yenye utamaduni wake hasa katika eneo la utimamu wa wachezaji na nguvu pamoja na kuwa tayari kuabdilika kulingana na mazingira. 

Hata hivyo Arsenal walikuwa na majanga mengine ikiwemo kadi nyekundu tano na kusababisha wachezaji hao kukosekana kwenye baadhi ya mechi. “Sitafuti kisingizio, sitaki tamaa kwani ninawapa nafasi wachezaji wengine kuonesha thamani yao na kutetea jezi za timu hii. Malengo yetu ni kushinda mechi zote zilizopo mbele yetu,”

Arsenal wanakutana na Real Madrid kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 15 ambapo walifanikiwa kutinga robo fainali mara mbili kwenye kipindi hicho. Mara ya mwisho Arsenal ilitinga nusu fainali msimu wa 2008/2009.

Kuwa bora kuliko wao

Arteta anaamini kuwa ushindi dhidi ya Real Madrid utapatikana ikiwa wao watakuwa timu bora uwanjani kuliko bingwa huyo mtetezi. Anasema kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho Arsenal wanapaswa kuwa makini na imara zaidi kuliko Real Madrid. Kocha huyo amesema kuwa mpango wao ni kuhakikisha wanacheza kana kwamba hawana tatizo lolote la kuondokewa na wachezaji muhimu akiwemo Gabriel Magalhaes. 

Anaeleza kuwa Arsenal wataingia uwanjani kupambana na timu hiyo bila kuhofia lolote kwani wanaelewa mazingira yao na wapinzani wao jinsi walivyo. Katika kuandaa mkakati huokocha huyo amebainisha utimamu na ari ya kusaka ushindi ndicho kitu ambacho anakitarajia kutoka kwa wachezaji wake.

Kutabirika na kutotabirika

Mikel Arteta amebainisha kuwa amegundua maeneo kadhaa ambayo yanatabirika kwa Real Madrid katika uchezaji wao, mbinu zao na wachezaji kwa ujumla. Amefichua kuwa yote hayo yanafahamika hivyo Arsenal watakuwa kwenye mpango maalumu wa kuibuka washindi. “maandalizi yetu yanahusiana na jinsi tutakavyofanya kwenye mchezo wowote, tunajiandaa wenyewe. Lakini linapokuja suala la kupambana na timu pinzani kama Real Madrid tunapaswa kujielekeza kwao, kwa aislimia fulani na vitu gani vinavyofanywa ili kupata ushindi dhidi yao. linapokuja suala la Real Madrid kuna sababu mbili; moja inahusiana na kisaikoloji zaidi, ni suala la hisia. Sababu ya pili inahusiana na kutabirika kwao namna wanavyofanya au kuwaandama wapinzani wao, na pia sababu ya tatu ni kutotabirika kwao, kwani wanaweza kufanya matukio ya kushangaza; mfano uwezo wao wa kutumia matukio hayo ya kustaajabisha ili kupata matokeo. Vitu kama hivi huwezi kuvifundisha, badala yake tunazungumzia kama vile kujiandaa endapo vitatokea na kujaribu kuvizuia. Lakini ni sehemu ya mchezo wao, wamezoea kutotabirika na kutabirika, ndiyo maana wamekuwa klabu kubwa.”

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version