Menu
in , , ,

“Simba lazima ishinde”-Ahmed Ally

Tanzania Sports

Leo hii mkuu wa idara ya habari ya klabu ya Simba SC , Ahmed Ally alikuwa eneo la Karume ambapo Tanzania Sports ilikuwepo kushuhudia ufunguzi wa hamasa ya Simba SC kuelekea mchezo wao wa kombe la shirikisho utakaochezwa Benjamin Mkapa jumapili ijayo.

Akizungumza kwenye hamasa hiyo, Ahmed Ally amezungumza masuala mbalimbali. Ahmed Ally amebainisha mambo yaliyotokea Libya na kipi ambacho wao kama Simba SC wanatazamia kwenye mchezo wa marudiano.

Tulikwenda Libya tukiwa na malengo matatu, lengo la kwanza ni kushinda mchezo, lengo la pili ni kutoka sare na lengo la tatu ni kufungwa kwa idadi ndogo ya magoli.  Alizungumza Ahmed Ally akizungumza na mashabiki wa Simba eneo la Karume.

Tunachoshukuru tumefanikiwa lengo la pili la kutoka suluhu. Matokeo ambayo yatakuwa na faida kwetu sisi kwa sababu tutakuwa nyumbani ambapo tutakuwa na faida ya mashabiki wetu.

Mechi ya Libya ilikuwa ni mechi ya wachezaji. Mechi ya hapa itakuwa mechi ya mashabiki. Mashabiki wetu ndiyo watakaoamua kama Simba SC itaingia kwenye makundi au la.

Mechi ya hapa haitokuwa nyepesi kwa sababu wapinzani wetu watafunguka kutafuta goli hawatokubali kukaa nyuma kwa sababu ya matokeo ya awali ya bila kwa bila lazima watafute goli.

Kila mwana Simba anatakiwa kukumbuka mechi ya ligi ya mabingwa barani Afrika ya mwaka 2018 dhidi ya Nkana Red Devil ambapo tuliwatoa pale Benjamin Mkapa.

Kila mwana Simba alikuja kwa wingi uwanjani na kuiwezesha Simba Sc kwenda hatua ya makundi. Ni nafasi nyingine mwaka huu kwa wana Simba kuibeba timu kuipeleka hatua ya makundi ya kombe la shirikisho.

Pia msemaji huyo amesema kuwa wao kama Simba wamefurahia matokeo yaliyotokea Libya kwa sababu yanapa nafasi ya kupindua matokeo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya martinkiyumbi@gmail.com

Leave a Reply

Exit mobile version