Menu
in

Simba kuzikosa alama tisini

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Simba SC imeambulia sare ya bila kufungana na Coastal Union katika mchezo uliofanyika uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.

Timu ya Simba iliingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya ushindi katika mzunguko wa kwanza,  ilihitaji ushindi ili ifike alama 87 huku wakitegemea mchezo wa mwisho endapo wakishinda timu hiyo ingekusanya alama 90.

Kwa matokeo haya endapo itashinda mchezo wa mwisho itafikisha alama 88 na ndio itakuwa mwisho wa msimu.

Katika mchezo huo ambao beki Pascal Wawa alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 74 baada ya kukaidi kipyenga cha muamuzi.

Coastal Union imefikisha alama 53 katika nafasi ya sita ikimshusha Kagera Sugar iliyo na alama 52.

Matokeo ya michezo mingine , Alliance FC imetoa sare ya kufungana magoli 2-2 dhidi ya Ndanda FC huku Lipuli ikipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting.

Wakati Polisi Tanzania imeambulia sare ya goli 1-1 dhidi ya  JKT Tanzania.

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

Leave a Reply

Exit mobile version