Menu
in , ,

Simba kuna vita kali, msimu utawaka moto

Tanzania Sports

Akiandika katika mitandao ya kijamii bilionea na mwekezaji wa Simba, Mohmammed Dewji amemsifu mlinda mlango kinda wa Simba Ali Salim

HAWAKUFUNGA goli ndani ya dakika 90, lakini mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu Tanzania, Simba wameonesha shauku kubwa na uzoefu katika mashindano ya Ngao ya Jamii. Mechi moja tu dhidi ya Singida FC imeonesha jinsi gani  Simba wanaweza kukabiliana na yeyote. Katika mchezo wao walilazimika kuigia hatua ya matatu ambako walishinda mabao penalti 4-2. TANZANIASPORTS imefanya tathmini kwa kuangalia masuala kadhaa muhimu yaliyojitokeza, kuanzia ndani ya uwanja hadi nje ya uwanja.

VITA YA KIUNGO WA KATI

Dakika 45 za kipindi cha kwanza kocha  wa Simba Robertinho alimtoa kiungo tegemeo Saido Kanoute na kumwingiza Fabrice Ngoma. Kuingia kwa Fabrice Ngoma kunabadili aina ya mchezo wa Simba na inaonesha namna nyota huyo alivyo mahiri katika kusoma mchezo wa wapinzani. Hii ni moja ya kazi ya mchezaji anayekaa benchi kuangalia mchezo kwa makini na kusomakuwa Saido Kanoute hapigi pasi ndefu, hapambani kimabavu, lakini ana akili nyingi sana. Saido Kanoute kwa misimu kadhaa amekuwa mhimili wa Simba akiwa na Mzamiru Yassin, lakini Fabrice Ngoma ameleta muono tofauti kikosini. Kwa hakika vita ya namba kwenye kiungo ni kali sana.

MABAO 100

Kama kuna mzigo mzito unaowakabili Simba ni safu ya ushambuliaji. Safu hiyo inatakiwa kufunga mabao 60 peke yao bila kutegemea viungo au mabeki. John Bocco, Osamba Onana, Jean Baleke, Moses Phiri, Kibu Dennis ni miongoni mwa washambuliaji ambao wanatakiwa kufunga mabao 20 kila mmoja ili kuipa uhai Simba. Washambuliaji hawa ndiyo tegemeo kikosi, na kwa vile ndani ya dakika 90 hawakuziona nyavu za wapinzani wao. Ikiwa Simba watamudu jambo hili Simba wanaweza kuandika rekodi ya aina yake. Kwanza wachezaji hawa wanao ushindani binafsi wa namba kikosini, pili wanafukuzia kupewa nafasi nyingi na kocha Robertinho, na tatu lazima wafunge ili wapewe nafasi zaidi. Kufunga mabao ndiyo kazi waliyopewa, hakuna mbadala.

GOLIKIPA WA VIWANGO

Akiandika katika mitandao ya kijamii bilionea na mwekezaji wa Simba, Mohmammed Dewji amemsifu mlinda mlango kinda wa Simba Ali Salim, lakini amekiri kuwa nafasi hiyo inamhitaji golikipa mwenye uwezo wa juu kushindana na Aishi Manula. Ushindani huo unalenga kuboresha eneo la golikipa. Katika mchezo wao wa Ngao ya Hisani, Ali Salum alikuwa shujaa wa mchezo baada ya kupangua penati ya kwanza iliyopigwa na Aziz Andambwile. Ali alidhihirisha kuwa uamuzi wa Simba kuatemana na Benno Kakolanya ulikuwa sahihi, kwani uhodari wake ni ndani ya dakika 90, lakini kwenye matuta hafui dafu.

Bado eneo hilo linahitaji huduma ya Manula ambaye amekuwa majeruhi kwa miezi kadhaa. Pamoja na hilo, Ali Salim alikuwa na wakati mzuri kwani safu ya ulinzi ya Simba imeimarika.

MAWINGA WATATOANA JASHO

Pape Sakho ameondoka, hii inatoa nafasi kwa Kibu Dennis kucheza upande wa kushoto au Moses Phiri. Wachezaji wawili hawa wanaweza kucheza upande wa kulia na kushoto na kuchangia uimara wa safu ya ushambuliaji. Lakini Peter Banda hajawa mchezaji wa kutumainiwa kwa misimu miwili sasa, lakini ana kipaji murua ambacho kinaweza kuivutia timu yoyote. Eneo la mawinga nalo linaweza kushuhudia moto mkali msimu ujao, kwa sababu kocha atakuwa na kila sababu ya kuvuna matunda ya nyota wake akiwemo Lous Miquessone aliyerejea kutoka Al Ahly ya Misri. Ni mchezaji kipenzi wa washabiki wa Simba, naye anaingiza moto mwingine kikosini.

BABU NA WAJUKUU ZAKE

Saido Ntibazonkiza anafahamika kwa jina la utani kuwa babu kwa sababu ya ukongwe wake. Mchezaji huyo anaweza kucheza winga wa kulia au kushoto, pamoja na kiungo mshambuliaji akiwa nyuma ya mshambuliaji. Tangu amejiunga na timu hiyo amekuwa mchezaji tishio na ametawala kwa muda. Wakati Saido akitawala kando yake kuna mfalme mwingine Cletous Chama. Nyota huyu mzambia ni kipenzi cha wana Simba, hawaambiliki. Na sasa amesogezewa mwanamfalme mwingine Louis Miquissone ambapo kwa pamoja walitengeneza ufalme wa kikosini mwa Simba. Katika hali hiyo ni wazi vita kali ya namba inaweza kumpunguzia dakika na majukumu Saido Ntibazonkiza. Hii ina maana vita vya ufalme ndani ya Simba zitazidi zaidi msimu ujao na huku kocha akiumiza kichwa kuchagua wa kuanza naye kwenye kikosi cha kwanza. 

MAKOCHA

Hapo ndipo uamuzi wa kocha unatakiwa kuchukuliwa kwa uangalifu ili asitie mchanga kitumbua chake. Anatakiwa kuhakikisha wacheaji wote wanatoa mchango lakini hasa wale wenye kuonesha ubora wao mechi mfululizo.  Ni kibarua kigumu kilichopo mbele ya benchi la ufundi huku kila mchezaji akionesha hamu ya kutawala kikosini.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version