Menu
in , , ,

Simba kuchaguana Juni 29…

WANACHAMA 41 wa Klabu ya Simba kutoka sehemu mbalimbali nchini wamerudisha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za klabu hiyo inayotarajia kufanya uchaguzi mkuu Juni 29 mwaka huu akiwamo beki na kocha msaidizi, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ anayewania cheo cha Makamu wa Rais.

 

Katika nafasi hiyo Julio aliyekuwa mgombea wa mwisho kurudisha fomu jana na mgombea pekee aliyetoa Dola za Marekani 200 kulipia ada ya Sh. 200,000 kulipia fomu anawania cheo hiko pamoja na Geofrey Nyange ‘Kaburu’, Swedy Mkwabi, Wilbrad Mayage, Joseph Itang’are na Benedict Kabulwa.

 

JULIO AJINADI YEYE NI BORA

Mara baada ya kuchukua fomu Julio alisema kuwa anauwezo wa kuingoza Simba na ana ni haki yake kama mwanachama wa klabuhiyo iliyoanzishwa tangu mwaka 1936.

 

Beki huyo alisema pia katika maisha yake ataendelea kuitumikia Simba kwa sababu ameifanyia mambo mengi ya maendeleo katika kila klabu inapokumbwa na migogoro ya uongozi.

 

“Hakuna ambaye anaweza kunishinda, ninaamini nina uwezo wa kuiongoza Simba, katika viongozi walioko madarakani robo tatu hawana uwezo na nimejiandaa kuwawekeza pingamizi,” alisema beki huyo mkongwe wa Simba.

 

KABURU

Mgombea huyu wa nafasi ya Makamu wa Rais alirejesha fomu yake saa 8:42 mchana na hakutaka kuzungumza maneno mengi wakati anakamilisha zoezi hilo.

“Hapa sio Siasa, ni kazi tu,” alisema kwa kifupi Kaburu ambaye anatoka katika kundi la Friends of Simba.

 

Kaburu pia ni Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Simba na mmoja wa wachezaji aliowasajili na walioifanyika kazi nzuri klabu hiyo ni Emmanuel Okwi na Ramadhan Messi ‘Singano’ ambaye sasa anawika kwenye kikosi cha kwanza.

 

MZEE KINESI

Licha ya kurejeshewa fomu na ndugu yake, Kinesi ni mmoja wa viongozi wanaoisaidia Simba katika kuendeleza programu zake za mazoezi kwa kutoa uwanja wake.

Hata hivyo Kinesi anatajwa kuongoza kikao kilichoitwa cha Mapinduzi cha kumng’oa Mwenyekiti, Ismail Aden Rage, yeye pamoja na wajumbe wenzake wa Kamati ya Utendaji.

 

MICHAEL WAMBURA

Katibu huyo wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania (FAT sasa TFF) alirejesha fomu yake ya kuwania Urais na baadhi ya wanachama wakimsindikiza.

 

Wambura aliitaka kamati ya uchaguzi kuangalia upya ratiba yake ya siku za kufanya kampeni akieleza kwamba siku nne hazitoshi kwa wagombea kuzunguka kunadi sera zao na kuomba kura.

 

“Dar es Salaam peke yake in a matawi 80, sasa kwa siku nne hazitoshi, na je katika mikoa kama Arusha, Mwanza, Shinyanga na Zanzibar ambayo ni sehemu ya Tanzania,” aliongeza Wambura.

Hata hivyo Wambura amekuwa akikutana na ‘vigingi’ kadhaa katika chaguzi anazotaka kushiriki kutokana na kuondolewa kufuatia kutotimiza sifa.

 

Wambura pia aliwahi kuongoza Simba kama Mwenyekiti wa Kamati ya Muda mwaka 2006 .

Wambura alifuatana na Julio na mara baada ya kukamilisha zoezi la kurudisha fomu, wanachama wawili waliofuatana waliwasomea dua ili waweze kufanikiwa katika harakati zao za kuwania uongozi ndani ya Wekundu wa Msimbazi.

 

WAGOMBEA WOTE WAREJESHA FOMU

Katibu Msaidizi wa Kamati ya Uchaguzi, Khalid Kamguna,alisema jana jioni kuwa wagombea wote wamerejesha fomu za kuwania nafasi saba zilizotangazwa na kamati hiyo.

Kamguna aliwataja wagombea wote waliorejesha fomu kuwa ni pamoja na Evans Aveva, Wambura, na Andrew Tupa wanaowania Urais.

 

Katika nafasi ya Makamu wa Rais watakaochuana ni waliochukua ni Kaburu, Joseph Itang’are, Swedi Nkwabi, Bundara Kabulwa, Willbard Mayage na Julio.

 

Wanaowania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ambazo ni nafasi nne zi Abdulhamid Mshangama, Alfred Martin, Ally Sulu, Iddy Kajuna, George Wakuganda, Said Tuli, Ramson Athuman, Seleiman Abdul, Khamis Mkom, Said Pamba, Rodney Chiduo, Collin Frisch, Chano Karaha, Emmanuel Kazimoto, Juma Pinto, Salim Jazaa, Yassin Said, Hussein Simba, Damian Manembe, na .

 

Wagombea wengine wanaowania nafasi hiyo ni Ally Chaurembo, Ibrahim Masoud, Ahmed Mlanzi, Iddi Nassoro, Kessy Kikoti, Maulid Said, Juma Mussa, Omary Said , Said Kubenea, Ramson Rutiginga na Khamis Mkoma.

 

Kamguna aliwataja wagombea wanawake wanne waliorejesha fomu ni pamoja na Asha Kigundula, Asha Muhaji, Jasmin Badar na Amina Hussein.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version