Menu
in , ,

Simba endeleeni kukubali kuitwa “underdogs”

Tanzania Sports

Wakati natazama “draw” ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika kuna kitu ambacho kilikuwa kinazunguka sana kichwani mwangu.

Ni timu ipi itapangiwa na Simba?. Hili ndilo swali kubwa ambalo lilikuwa linapita kichwani mwangu.

Nilikuwa najiuliza siyo kwamba nilikuwa najua nina shauku kubwa sana ya kujua ni timu ipi itacheza na Simba katika hatua hiyo.

La Hasha!, kichwani mwangu nilikuwa najiuliza swali moja tu, je Simba wameshakuwa wakubwa kwenye michuano hii au bado ni underdogs?

Hiki ndicho kilikuwa kinazungukwa kichwani mwangu ?. Kwanini ?, jibu ni moja tu. Simba wakati wameingia kwenye hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika kuna mjadala mkubwa ulikuwa unaendelea.

Mjadala wa kuwa Simba ni “Underdogs” au siyo “Underdogs” wa kundi. Huu ndiyo ulikuwa mjadala mkubwa sana.

Na inawezekana kwa kiasi kikubwa mjadala huu ndiyo ulioipa nguvu kubwa sana Simba kupambana ili kulikataa hilo jina.

Kitu ambacho ni kizuri, siyo kibaya. Na inaonekana Simba wamepata mafanikio makubwa sana ambayo wengi tunajivunia nacho.

Turudi kwenye hoja. Wakati natazama ile draw nilikuwa nawatazama wapinzani ambao walitakiwa kukutana na Simba katika hatua ya robo fainali.

Mpinzani wa kwanza alikuwa Esperance ya Tunisia. Huyu ndiye bingwa mtetezi wa ligi ya mabingwa barani Afrika.

Bingwa mtetezi, siyo timu timu ya kubeza hata kidogo. Tuachane na Esperance. Timu nyingine ilikuwa Wyadad ya Morocco.

Huyu ni bingwa aliyepita wa kombe la shirikisho barani Afrika msimu uliopita. Timu ya tatu ilikuwa TP Mazembe.

Ambaye msimu juzi alikuwa bingwa wa kombe la shirikisho barani Afrika. Na alishawahi kuwa bingwa wa ligi ya mabingwa Afrika.

Kwa kifupi Simba alitakiwa kukutana na mabingwa. Watu ambao wamewekeza kwenye hili kombe na wako na nia nalo kabisa.

Kivyovyote vile na hapa kwenye hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika , Simba alikuwa underdog mbele ya hizi timu tatu.

Hakuna timu moja ambayo analingana nayo mabavu kati ya hizo timu tatu. Hakuna. Yeye ni mtoto mdogo sana mbele ya hizo timu.

Hata alipopangiwa na TP Mazembe watu wengi waliona TP Mazembe wamepata mteremko kuelekea hatua ya robo fainali.

Kwa hiyo kwa tafasri ya haraka haraka hapa Simba ni Underdogs kwenye hii mechi. Kitu ambacho ni kizuri sana na anatakiwa akubaliane nacho kabisa.

Hatakiwi kujiona mkubwa tayari kwa sababu tu amefika hatua ya robo fainali. Kuwa mkubwa kuna hatua ambazo mtu anatakiwa kuzifikia.

Bado hajawa mtu mkubwa, na anapoingia kwenye hii mechi pia anatakiwa kufahamu kuwa yeye ni mdogo.

Hatazamwi kama mtu anayeenda kushinda hii mechi. Anatazamwa kama mtu ambaye anaenda kuwa mteremko.

Kitu hiki kinafaida kubwa sana kwa Simba!. Wanachotakiwa ni wao kukubaliana nacho na kinaweza kuwanufaisha kwa kiasi kubwa.

Kitawanufaisha kwa njia ipi ?. Simpo tu. TP Mazembe wataingia kama watu ambao wanatazamwa kuwa washindi kwenye hii mechi.

Kwa hiyo kivyovyote vile presha kubwa itakuwa ndani yao kuliko kwa Simba. Wao watatakiwa kudhibitisha ukubwa wao, kwa hiyo wataingia kwa nguvu kudhibitisha hilo.

Presha ikiwa kubwa ndani yao watalazimishwa kufanya makosa tu. Na Simba wakiwa hawana presha kubwa ndani yao hawatafanya makosa makubwa ndani ya uwanja.

Kwa hiyo Simba kukubali kuwa Underdog kutawafanya wawe na presha ndogo ambayo itawafanya wasifanye makosa binafsi ndani ya uwanja.

Hii ndiyo silaha ya kwanza kwa Simba kuweza kushinda hii mechi, wao kuwa underdogs kutawasaidia sana kuliko kujiona wakubwa ndani ya hii mechi.

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya martinkiyumbi@gmail.com

Exit mobile version