Taarifa ambayo tayari imeenea kupitia mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari juu yakujiengua kwa Mtendaji Mkuu wa Simba SENZO Mazingiza .
Hii taarifa imeanzia Twitter kabla ya kusambaa Instagram na kuenea sehemu mbalimbali kila mmoja amestaajabu nini kimeendelea.
Tatizo kubwa linalosemekana kujiondoaa kwa Senzo ni usajili wa nyota Benard Morrison na kutaka kuondolewa kwa kocha wa timu iyo Sven Vandenbroeck.
Hoja ya Senzo hakutaka usajili wa Morrison huku viongozi bado wanavutana kumuondoa Sven.
Siku ya jumapili mchana ndio taarifa ya kuondoka kwake ikatokea akiwaaga wanasimba kwa kumpa nafasi yakufanyakazi.
Ikumbukwe ndio kwanza miezi 9 tangu ajiunge na Simba akitokea Afrika kusini katika timu ya Orland Pirates .
Ameandika kupitia twitter “ Nawashukuru uongozi wa Simba kwa kunipa nafasi kuongoza timu hii kubwa, nachukua nafasi hii kujiondoa katika timu hii ambapo kwa muda mchache timu imepata mafanikio sana,” aliandika.
Hii imekuja siku moja baada ya kutangazwa kwa aliyekuwa mchezaji wa Yanga Benard Morrison kujiunga na Simba hivyo kama amekuja kuharibu hali ya hewa.
Tetesi zinasema kuwa Yanga wapo katika muda sahihi wa kuongea naye ili ikifika katika mabadiliko basi waanze kuwa naye.