Menu
in , , ,

Saudi Arabia na hadhi ya kuwa kitovu cha soka

Tanzania Sports

Saudi Arabia haina hadhi ya kijamii wala kisiasa kuwa kitovu cha soka duniani

Nchi hiyo ni tajiri kifedha na kimatamanio. Mwana mfalme wao, Mohamed bin Salman, anasema kwamba nchi yake itageuka kuwa ‘Ulaya mpya katika kipindi cha muongo mmoja. Soka ni moja ya mikakati yake muhimu. Anataka kushindana kwenye Ligi ya Mabingwa, hivyo anawekeza sana kwenye wachezaji waliokuwa nyota wakubwa wa Ulaya.

Cristiano Ronaldo, Neymar na Karim Benzema sasa wanacheza na kupata mishahara ya ‘kufuru’ nchini Saudi Arabia. Wengine wachache ambao wamevuka umri wa miaka 30 bila shaka watawafuata huko.

Linaelekea kuwa dili linalokamilishwa ili kuona kwamba Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanaume 2034 zikafanyika nchini Saudi Arabia. Japokuwa mchakato unaendelea, Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino kimsingi ametangaza hivyo kwenye akaunti yake ya Instagram.

Wadhamini wapya wakau wa FIFA, Aramco, wanamilikiwa na Taifa la Saudia, ambapo pengine hicho ni kiashiria kingine kwamba taasisi hiyo inaangalia zaidi masuala ya fedha linalokuja kugawa umiliki wa fainali. Unatakiwa kuwa na uwezo wa kumudu miradi ya hivyo.

Qatar inadaiwa kutumia zaidi ya $200bn (£159bn) kwa ajili ya fainali za 2022 za Kombe la Dunia. Mashindano hayo yatagharimu pungufu zaidi baada ya  miaka 11, hasa kwa kuwa ni timu 48 badala ya 32 zitakazoshiriki.

Kwenye miaka 10 hivi iliyopita, nchi nyingine ilijaribu kufuatisha maslahi ya kijiografia na kisaiasa kwenye soka. China walianza kununua wanasoka ambao umri ulikuwa ukienda kutoka Ulaya kwa kiasi kikubwa cha fedha, Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti, Xi Jinping alitaka kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la wanaume, na akaweka lengo la China kuwa mabingwa wa dunia.

Kisiasa, China ni muhimu lakini husikii lolote juu ya soka. Hufanya kazi tu pale ambapo ushiriki unawezekana kwa kila mmoja, ambapo kujitolea kujenga jamii inayojitambua kidemokrasia na hicho hakijengwi kwa usiku mmoja. Huhitaji zaidi ya fedha na nyota kutoka nje ili kuweza kwenda na kasi ya soka ya Ulaya.

Mizizi yake ipo Glasgow, Sheffield, Geneva, London, Budapest, Barcelona, Milan, Nuremberg na Vienna, huku majani yake yakichipulia Buenos Aires na Montevideo. Ulaya wangeweza kuja na kitu – na ingekuwa bora – kuanzisha ya kwake dhidi ya Marekani, hasa kwa vile Amerika Kusini, bara la pili kwa ubora zaidi wa soka baada ya Ulaya wapo karibu.

Mwanasoka wa Argentina au Brazil asingehitaji tena kwenda Hispania au Ureno, bali akaenda San Francisco, Atlanta au Miami. Wengi wanaweza kujitambulisha kirahisi ziadi hivi kuliko Riyadh.

Saudi Arabia wamefuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mara sita..ndiyo nchi kubwa zadi kwenye eneo lao hilo, ikiwa na wakazi milioni 36. Idadi ya watu bado ni ndogo. Kuna maslahi ya soka, na washabiki wake kwa maelfu walisherehekea sana ushindi wao dhidi ya Argentina nchini Qatar. Saudi Arabia wangeweza kustahili nafasi. Lakini ni kwa namna tofauti kisiasa, kwa sababu utamaduni wa soka huleta ubinadamu.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version