MIAKA mingi iliyopita ilikuwa vigumu kuona timu za Tanzania zinafurukuta katika mashindano ya Kimataifa hasa pale zinapopangwa dhidi ya timu za Afrika kaskazini au Afrika magharibi. Linakuwa jambo la kusisimua pale unapoona mkwaju mkali wa Jean Ahoua wa Simba dhidi ya Sfaxien ya Tunisia na kuihakikisha Simba ushindi wa 1-0 ugenini. Kwa wanaofahamu kandanda Afrika klabu ya Sfaxien ni miongoni mwa vigogo wa Kiarabu pamoja na vingine vilivyowahi kutesa kwenye mashindano mbalimbali ya CAF.
Daraja la Sfaxien ni lile la Al Ahly, Raja Casablanca, JS Kabylie,Wydad Casablanca, Esparence, USM Alger, Club Africain pamoja na wengine kama vile Stella Abdijan, Heats of Oak,TP Mazembe, Mamelodi Sundowns, AS Vita, Sport Club Villa, Gor Mahia, ASEC Mimosas kwa kutaja chache. Ukiangalia jinsi timu za waarabu na vigogo wanavyoteseka kwenye mashindano ya CAF unabaki unatabasamu hasa pale timu za Tanzania zinapotoa somo zuri sana ‘kutesa kwa zamu’.
Nini kimebaidlika haraka?
Miaka mingi mchezaji wa Tanzania hakuwa na fasi ya kusajiliwa moja kw amoja na vilabu vya Waarabu. Mara nyingi mchezaji aliyekwenda huko ilikuwa kufanya majaribio. Wengi waliotaka kuondoka lakini mazingira yaliwanyima fursa. Wachezaji wa Kitanzania walikuwa wanajaribu kupenya kwenye ligi za Afrika na hata Ulaya, kwa sababu Oman kulikuwa kama sehemu isiyo na kiwango tofauti na sasa.
Lilikuwa jambo gumu kuona kocha mweusi anateuliwa kufundisha timu za waarabu. Ndiyo maana Pitso Mosimane anakuwa kocha wa aina yake ambaye aliweka misingi na kuonesha ubabe wa namna ya kuwa kocha mzuri na kwmaba makocha wazuri wapo tela kusini mwa jangwa la sahara. Rhulani Mokwena na Fadlu Davids ni miongoni mwa makocha kutoka kusini mwa jangwa la sahara ambao wamefanya vizuri kwenye kazi zao wakiwa kwenye klabu za Waarabu.
Unapoona mchezaji kama Simon Msuva au Nikcosn Kibabage ananunuliwa moja kwa moja kutoka Tanzania kwenda Morocco ni lazima utajiuliza swali nini kimebadilika kwa mwarabu?
Ni dhahiri soka la nchi za Waarabu linakosa wachezaji mahiri wa ndani. Miaka ya nyuma walikuwa wanasajili wachezaji wengi weusi kutoka Afrika magharibi. Wachezaji wa Afrika magharibi walikuwa na soko, na hata sasa bado wanalo lakini si idadi kubwa kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Rudisha kumbukumbu kwa mwamba Julius Aghahowa ambaye alitesa Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na Esperance kisha akanunuliwa kwenda Ufaransa. Vilabu vya Ufaransa vilikuwa na watafuta wachezaji wao na walilenga zaidi kwenye nchi za Kiarabu.
Hata hivyo wimbi la upungufu wa wachezaji mastaa na wenye viwnago vikubwa kutoka Afrika magharibi limesababisha timu za Kiarabu zishindwe kuziba pengo la upungufu wa vipaji vya ndani katika nchi zao. Unazitama Raja Casablanca ikicheza na Mamelodi Sundowns unagundua kabisan wanakabiliwa na tatizo la vipaji vya kandanda. Wakati Mamelodi Sundowns wakicheza mpira kadiri wanavyojisikia, lakini Raj Casablanca wanapiga pasi tatu hadi nne kwenda golini mwa adui.
Ule mpira mkali kutoka nchi za Kiarabu umedorora kwa kiasi kikubwa. Ukiwaangalia Simba walivyotawala Sfaxien unakumbuka wazi kuwa hali wanayopitia ni kama ile ya Manchester United. Sfaxien si timu ya kubezwa lakini hali ya sasa ni sawa na kukopa neno la vijana wa mjini “timu mdebwedo”. Timu hii si ile iliyokuwa tishio kama Esperance, Club Africain, TP Mazembe na kadhalika. Unaweza kuifikiria Al Ahly iliyolazimika kumununua Luis Misquisson wa Simba kwa sabahu walitaka kufanya kitu kinachofanywa na timu nyingi za Tunisia, Algeria na Morocco kuwanunua wachezaji wenye vipaji kutoka nchi za Afrika magharibi na sasa afrika mashariki.
Miaka ya nyuma Luis Miquissone angeambiwa akafanye majaribio kule Misri. Himd Mao naye alinunuliwa kutoka Tanzania na amekuwa mmoja nguzo na alama muhimu katika Ligi Kuu Misri. Miaka ya nyuma haikuwa rahisi kuona kitu hiki. Ni dhahiri soka la waarabui limeshuka mno na walichobakiza kwenye timu za Taifa ni kutegemea watoto wao waliozaliwa huko Ulaya ili warudi nyumbai kuchezea nchi zao.
Ni ipi siri kuibuka kusini mwa jangwa la sahara?
Bravos ni miongoni timu zinatisha kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu, na wapo kundi moja na Simba wkaiwa na pointi 6. Simba nao wana pointi 9 kwahiyo wanamtetemesha Sfaxien ambaye yuko hoi kwenye kundi lao. Kimsingi mabadiliko katika uendeshaji wa Ligi yamechangia timu hizi kuongezeka nguvu pamoja na uwezo wa kusajili wachezaji wengi wa kigeni.
Wachezaji wa kigeni wameona soko katika ukanda huo hivyo wamefanikiwa kutangaza vipaji vyao kwa mafanikio. Mafano Afrika mashariki wachezaji wengi wa kigeni wanatamani kuja kucheza hapa kwa sababu wana uhakika timu zetu zinashiriki mashindano ya Kimataifa hivyo nao kutangaza vipaji vyao. Ongezeko la wawekezaji kwenye Ligi za ndani kumechangia kuinua kiwnago cha uchumi cha vilabu na kuweza kushindana na wengine kiwanjani.
Pengine uwezo wao kiuchumi si mkubw akama timu za Waarabu lakini vipaji vyao hatuwezi kuvibeza. Kuna vipaji vinaonekana na kuwazidi maarifa timu za Waarabu kiasi kwamba unagundua kuwa wachezaji waliona kwenye timu hawana kitu cha ziada kuwazidi hawa walioko Simba, Yanga, Bravos, Mamelodi, Orlando Pirates au Petro Atletico na kadhalika.
Je nguvu hiyo italeta makombe?
Rekodi zinaonesha timu za Waarabu ndizo zimetwaa amkombe ya CAF mara nyingi zaidi kuliko zingine. Al Ahly, Zamalek, Esperance, Sfaxien, Raja, Wydad Berkane kwa kutaja chache ni miamba ambaye imetamba na kutwaa mataji Afrika. Katika timu zinazoibuka kusini mwa jangwa la sahara au afrika magharibi, rekodi zao kutwaa mataji zipo chini mno.
Lakini kiwnago chao katika kandanda kimebadilika na kutanua wigo kuliko miaka ya nyuma. Ukiondoa Mamelodi Sundowns ya Pitso Mosimane iliyotwaa Ligi ya Mabingwa na Mamelodi Sundwons ya Rhulani Mokwena iliyotwaa African Football League, timu zingine hazina rekodi nzuri ya kuchukua makombe. Hiki ndicho kilichobakizwa na ambacho kitaongeza thamani zaidi kwa timu zetu. Ni wakati wa ushindani wa haki na hakuna kulala kizembe.