Menu
in ,

Rooney kuhamia China?

*Wakala wake atua kwa dili la £ mil 1 kwa wiki
*Benki ya China yataka kuinunua Southampton
*Barca wawawinda Hector Bellerin na Walker

Tetesi kubwa mjini kwa sasa ni kwamba Nahodha wa Manchester United na
Timu ya Taifa ya England, Wayne Rooney anakwenda zake China.
Kwamba safari yake Man U inafikia tamati na si ajabu ndani ya mwezi
mmoja akawa hayupo tena Old Trafford, kwani dirisha la usajili China
linaelekea ukingoni.

Katika kukoleza tetesi hizo, imeelezwa kwamba wakala wa Rooney, Paul
Stretford amekwenda China kwa ajili ya kuzungumza na klabu kadhaa za
Ligi Kuu ya China kukamilisha dili la Rooney.

Akifanikisha mipango ilivyo ni kwamba Rooney anayelipwa zaidi ya pauni
250,000 kwa wiki, atalipwa pauni milioni moja na kuwa mchezaji
anayelipwa zaidi duniani.

Wakala huyu kwa sasa yupo jijini Tiajin ilipo klabu ya Tiajin
Quanjian, moja ya zile zinazomsaka mshambuliaji huyo aliyeshuka
kiwango Old Trafford na anayepata muda mfupi wa kucheza kutokana na
ujio wa Zlatana Ibtahimovic.

Stretford alikwenda China majuzi na akafikia kwenye Hoteli ya
Renaissance alikofanya mazungumzo na maofisa wa klabu mbalimbali.
Stretford alipoulizwa na SunSport majuzi juu ya Rooney na safari yake
alijibu: “Kwa sasa mambo bado, hatuna taarifa rasmi kumhusu Wayne
Rooney katika hatua hii.”

Hata hivyo, kocha wa timu hiyo, Fabio Cannavaro alikiri kuwasiliana na
Rooney. Tayari Rooney (31) ameambiwa anaweza kuondoka Old Trafford
akipenda na kwa ukubwa wa dili hilo, kuna dalili za kuondoka kwake.

Hata hivyo, anaweza pia kuamua kubaki hadi mwishoni mwa msimu kama
heshima kwa klabu aliyotumikia kwa mafanikio makubwa na sasa anashika
rekodi ya mfungaji bora katika historia yake.

Could Hector Bellerín be off to Catalonia?

Kocha Jose Mourinho alipoulizwa juu ya Rooney, alitaka mchezaji huyo
aulizwe mwenyewe na si juu ya kocha kujua, kwani yeye mwenyewe
Mourinho hajui ikiwa atakuwa klabuni hapo wiki inayofuata.

Katika hatua nyingine, kuna benki ya China ipo tayari kutoa pauni
milioni 225 ili kuichukua kimoja klabu ya Southampton, ukiwa ni muda
mfupi baada ya kampuni nyingine ya Mashariki ya Kati kushindwa kufanya
hivyo.

Barcelona wanajipanga kwa ajili ya kumnunua beki wa kulia wa Arsenal,
Hector Bellerin, 21. Raia huyo wa Hispania alikuwa La Masia – akademia
ya Barcelona na sasa anawika Emirates katika kikosi cha kwanza.

Barca pia ambao ni mabingwa wa la Liga, wanataka kumchukua beki wa
kulia wa Tottenham Hotspur, Kyle Walker, 26, ikiwa chaguo la awali
litakwama.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amemsifu mchezaji wa Ajax katika
nafasi ya ushambuliaji, Kasper Dolberg, akionesha kutaka kumnunua kwa
sababu ni mzuri sana uwanjani.

Matarajio ya kumpata tena uwanjani kiungo wake mahiri, Santi Cazorla,
32, aliyekuwa majeruhi yamepukutika baada ya kutopona vyema na sasa
atasubiri hadi msimu ujao.

Alitarajiwa arejee kwenye mazoezi na mechi mapema lakini matibabu
yamechukua muda mrefu, ikiwa ni pamoja na upasuaji kadhaa, kama
kuondoa nyama mkononi na kuibandika kwenye enka alikoumia.

Arsenal na Manchester United walimtuma maskauti wao kumwangalia
mshambuliaji mwenye umri wa miaka 21, Andre Silva katika klabu ya
Porto ya Ureno.

Klabu ya Ligi Kuu ya China, Shandong Luneng wanataka kumsajili winga
wa Manchester United, Ashley Young, 31.

Mlinzi wa zamani wa Blackburn na QPR, Christopher Samba, 32, anafanya
mazoezi na wachezaji wa Aston Villa. Samba kwa sasa ni mchezaji huru
aliyeondoka klabu ya Ugiriki ya Panathinaikos.

Wakala wa mchezaji nyota wa Celtic, Moussa Dembele, 20, anasema
Mshambuliaji huyu wa Ufaransa hana mpango wowote wa kuondoka klabu
hiyo ya Uskochi.

AC Milan wanataka kumsajili kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas, 29.
Spurs wamemchukua golikipa Mdachi mwenye umri wa miaka 15, Nick
Weegink kumfanyia majaribio. Tineja huyu ambaye kwa kawaida huwa

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Exit mobile version