Menu
in , , ,

Robben: Man U kama mpira wa mikono

Winga wa Bayern Munich, Arjen Robben amewafananisha Manchester United na timu ya mpira wa mikono kwa jinsi walivyolinda lango lao karibu muda wote wa pambano Jumanne hii.

Nyota huyo hatari alisema kwamba wao kama Bayern walitaka kutandaza soka safi lakini wenzao wakawazuia kabisa huku wakisonga mbele tu kwenye mashambulizi ya kushitukiza baada ya kukabiliana nao.

Robben alidai kwamba katika mechi hiyo ambayo Bayern walitawala kwa asilimia 74, Man U waliufananisha kabisa mchezo huo na mpira wa mikono ambapo timu hukabili namna hiyo. Katika mpira wa mikono, mbinu hizo hutumika golini kuzuia fursa za washambuliaji kupata bao badala ya wanaoshambuliwa kutafuta kutawala mchezo.

“Haikuwa rahisi kwa sababu Manchester United walicheza kwa kujihami zaidi na hawakuacha pengo lolote,” akasema Robben ambaye alichezea Chelsea kati ya mwaka 2004 na 2007.

Kocha Pep Guardiola wa Bayern aliunga mkono maoni ya Robben, akisema kwamba ukishaona ni kipindi cha pili halafu wachezaji tisa wamo ndani ya boksi la goli lao si rahisi na kwamba ilikuwa muhimu kuutawala mchezo, kuwa wavumilivu na kupata walau bao moja. Timu hizo zilikwenda sare ya 1-1.

Kiungo wa Bayern anayedaiwa kutaka kwenda Manchester, Toni Kroos, aliyecheza dakika 74 kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Mario Gotze anasema kwamba japokuwa alivutiwa na Old Trafford kamwe hatashinikiza kujiunga nao. Alikiri kwamba dimba lao ni zuri lakini anachojua yeye ni mtu wa Bayern Munich.

Kroos (24) anamaliza mkataba wake na Bayern kiangazi cha 2015 na hadi sasa hajakubaliana dili la kuongeza mkataba wake huo na Wajerumani, lakini alipata kusema anataka kucheza Ligi Kuu England. Baada ya kusuasua kwa United ambao hawana uhakika wa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, Kroos alinukuliwa akisema angependa timu kama hiyo.

Mwenyekiti wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge amesema kwamba mchezaji huyo lazima amalizie mkataba wake hapo Allianz Arena, hivyo kuondoa matumaini yoyote kwamba Kocha David Moyes angeweza kumpata kwa ajili ya msimu ujao.

51.556732-0.117801

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version