Menu
in

Rekodi Za Yanga Na Simba Tangu 1965

Simba na Yanga uwanjani

Simba na Yanga uwanjani

Yanga na Simba zilianzishwa mwaka 1935 na 1936 baada ya kutokea mvurugano baina ya viongozi wa pande hizo mbili.

Yanga ndio timu kongwe zaidi Tanzania ilianza 1935 wakati Simba ikitokea ubavuni mwa Yanga baada ya mvurugano huo na kuunda timu nyingine inayoitwa Sunderland.

Lengo sio kutaja historia bali kuwakumbusha ubingwa wa Tanzania bara timu gani zimechukua tangu itambulike na kuitwa ligi kuu Tanzania Bara.

Ligi kuu Tanzania Bara rasmi ilianzishwa mwaka 1965 baada ya miaka minne ya Uhuru wa Tanzania ndipo ligi hiyo ilianzishwa.

Yanga na Simba ndizo zilizo chukua ubingwa mara nyingi zaidi kuliko nyingene zote hapa Tanzania Bara.

Ikiwa timu zote mbili zimechukua mara 48 wakati mara 6 pekee ndio zimechukua timu nyingine.

Timu nyingine zilizochukua katika miaka 54 ya ligi kuu Bara ni pamoja na Coastal Union, Tukuyu Stars, Azam FC na Mtibwa Sugar ambayo imechukua mara mbili.

Timu  za Simba na Yanga ndizo timu zilizochukua ubingwa mara nyingi kuliko timu nyingine nchini tangu mwaka 1965 mpaka 2020 kama nilivyotangulia kusema huko juu. 

Yanga ndiyo iliyochukua mara nyingi zaidi ubingwa huo ikifuatiwa kwa karibu na Simba ambayo zamani ilijulikana kama Sunderland Sports Club.

Yanga imechukua mara 27 Simba mara 21 mchuano ni mkali kweli kweli.

Msimu huu wa mwaka 2017/18 mbio zinaonekana kuwa mikononi mwa timu mbili za Simba na Yanga ambapo Simba walionekana kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuuchukua ubingwa wa msimu huo na kweli ilichukua.

Mwaka huu bado mambo magumu sana haijulikani timu ipi itavuna na ipi itaambulia mabua, Yanga , Simba na Azam FC ndizo zinazonekana kuwa karibu na taji hilo msimu huu.

Hapa chini tumekuwekea orodha kamili ya historia ya ubingwa huo tangu mwaka 1965:

Hapa sasa utagundua hii ya kuchukua mara nyingi kumbe ilianza muda mrefu na huwa Yanga na Simba wanalipana timu hiz ziliwahi kuchukua ubingwa mara tano mfululizo na nyingine mwaka uliofuata ikachukua mara hizo hizo.

Tuanze na msimu wa mwaka 1965 Sunderland (Simba SC), 1966 Sunderland, 1967 Cosmopolitan.

Baada ya hapo Yanga iliichukua mara tano mfululizo yaani 1968 Young Africans , 1969 Young Africans, 1970 Young Africans , 1971 Young Africans , 1972 Young Africans, 1973 Simba SC, 1974 Young Africans, 1975 Mseto SC.

Simba ililipa kuchukua mara tano mfululizo 1976 Simba SC, 1977 Simba SC, 1978 Simba SC, 1979 Simba SC, 1980 Simba SC, 1981 Young Africans, 1982 Pan Africans, 1983 Young Africans, 1984 Simba SC, 1985 Young Africans, 1986 Tukuyu Stars, 1987 Young Africans, 1988 Coastal Union, 1989 Young Africans, 1990 Simba SC, 1991 Young Africans, 1992 Young Africans, 1993 Young Africans, 1994 Simba SC, 1995 Simba SC, 1996 Young Africans , 1997 Young Africans na  1998 Young Africans .

Mtibwa imeingia katika historia kwa kuchukua ubingwa Karne ya 20 na 21 yaani 1999 Mtibwa Sugar na 2000 Mtibwa Sugar

Wakati  2001 Simba SC, 2002 Young Africans , 2003 Simba SC, 2004 Simba SC, 2005 Young Africans , 2006 Young Africans, 2007 Simba SC, 2007/08 Young Africans , 2008/09 Young Africans, 2009/2010 Simba SC, 2010/2011 Young Africans Sc, 2011/2012 Simba SC, 2012/2013 Young Africans Sc, 2013/2014 Azam FC, 2014/2015.

Yanga wamerudia tena kuchukua mara tatu mfululizo  Young Africans, 2015/ 2016 Young Africans , 2016/ 2017 Young Africans .

Mapigo ya kuchukua mara tatu mfululizo yamerejea kwa Simba nao 2017/ 2018, 2018-19, 2019-20.

Swali linabaki pale pale msimu huu timu ipi itachukua ubingwa kulingana na usajili wa wachezaji bora kwa vikosi vya Simba, Yanga na Azam.

ILI UZIONE VIZURI ANGALIA HAPA

1965 Sunderland (Simba SC)

1966 Sunderland

1967 Cosmopolitan

1968 Young Africans

1969 Young Africans

1970 Young Africans

1971 Young Africans

1972 Young Africans

1973 Simba SC

1974 Young Africans

1975 Mseto SC

1976 Simba SC

1977 Simba SC

1978 Simba SC

1979 Simba SC

1980 Simba SC

1981 Young Africans

1982 Pan Africans

1983 Young Africans

1984 Simba SC

1985 Young Africans

1986 Tukuyu Stars

1987 Young Africans

1988 Coastal Union

1989 Young Africans

1990 Simba SC

1991 Young Africans

1992 Young Africans

1993 Young Africans

1994 Simba SC

1995 Simba SC

1996 Young Africans

1997 Young Africans

1998 Young Africans

1999 Mtibwa Sugar

2000 Mtibwa Sugar

2001 Simba SC

2002 Young Africans Sc

2003 Simba SC

2004 Simba SC

2005 Young Africans Sc

2006 Young Africans Sc

2007 Simba SC

2007/08 Young Africans Sc

2008/09 Young Africans Sc

2009/2010 Simba SC

2010/2011 Young Africans

2011/2012 Simba SC

2012/2013 Young Africans

2013/2014 Azam FC

2014/2015 Young Africans

2015/ 2016 Young Africans

2016/ 2017 Young Africans

2017/ 2018 Simba

2018-19 Simba

2019-20 Simba

2020-21 ???

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

Leave a Reply

Exit mobile version