Menu
in , , ,

Real Madrid wamechelewa


*Borussia Dortmund watinga fainali Ulaya
*Bayern wawadai Barcelona mabao manne

Walicheza soka safi, ya nguvu na kutafuta ushindi, lakini jitihada zao zilikuja zikiwa zimechelewa na wameshajeruhiwa.
Real Madrid walijaribu kuweka historia lakini muda haukutosha, na ikadhihirika kwamba biashara huwa ni asubuhi na jioni ni mahesabu tu.
Baada ya kukung’utwa mabao 4-1 jijini Dortmund na Borussia Dortmund kwenye nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki iliyopita, wameishia kuwafunga Wajerumani hao 2-0 jijini Madrid.
Vijana hao wa Jose Mourinho ‘The Only One’ walianza mechi ya marudiano kwa kasi, wakipata kona na kulenga shabaha lakini ilikuwa ngumu kupata bao.
Walikuwa wakihitaji mabao matatu ili wasonge mbele kwa faida ya bao moja la ugenini, lakini Cristiano Ronaldo na wenzake walikuwa kama wana kigugumizi cha kutumbukiza mipira kimiani.
Hadi nusu ya kwanza Real wangeweza kuwa mbele kwa mabao matatu, lakini tafuta tafuta yao iliwachukua hadi dakika ya 82 kupata bao la kwanza, kupitia mchezaji aliyeingia kipindi cha pili, Karim Benzema.
Usiku wa Jumanne uligeuka wa shauku baada ya Sergio Ramos kufunga bao la pili dakika ya 88, huku Ronaldo akinyimwa penati aliyodhani ingekuwa halali na pengine kubadili kabisa matokeo ya mchujo wa fainali.
Mwamuzi Mwingereza Howard Webb alikuwa na kazi ngumu mbele ya mashabiki 76,000, wengi wao wakiwa wa Real, ambapo alianza kwa kujizuia kutoa kadi, kabla ya kuziachia kama njugu, ambapo hadi mwisho Real walipata nne na Dortmund tatu.
Kwa matokeo hayo, Dortmund wameingia fainali, na wanasubiri mshindi wa mechi ya Jumatano kati ya Barcelona na Bayern Munich.
Upo uwezekano wa fainali itakayochezwa Wembley jijini London kuhusisha timu za Ujerumani, kwani Bayern waliwanyuka Barca mabao 4-0 kwenye nusu fainali ya kwanza, na kuitia doa soka ya Hispania.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version