Menu
in , , , ,

Real Madrid kuwafukuza nyota wao

Tanzania Sports

NI dhahiri klabu ya Real Madrid imedhamiria kufanya mabadiliko makubwa ambapo ipo tayari kuwafukuza baadhi ya nyota wake ili kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao. Timu hiyo ipo kwenye mashindano matatu msimu huu, ambapo katika mchezo wa fainali ya Copa De Rey itapambana na mahasimu wao Barcelona, huku ikikabiliwa na kibarua kigumu cha kuchuana na Arsenal kwenye hatua ya robo ya roba fainali ya Ligi ya Mabingwa jumatano wiki hii. 

Real Madrid wameandaa mpango maalumu ambapo wachezaji waandamizi wanatarajiwa kuondolewa mwishoni mwa msimu huu ikiwa ni sehemu ya mabadiliko yanayofanywa na uongozi wa klabu hiyo. Baadhi ya nyota wa klabu hiyo ambao wana rekodi za kipekee wanategemewa kuruhusiwa kuondoka baada ya kucheza kwenye dimba la Santiago Bernabeu kwa miaka mingi huku wakiwa  wameweka alama chanya kwa kutwaa mataji mbalimbali.

Real Madrid inatarajiwa kuwa na jukumu kubwa la kusajili wachezaji wapya wa kuimarisha kikosi chao, huku mkononi wakiwa na Trent Alexandre Arnodl wa Liverpool. Beki huyo w akulia atajiunga na Real Madrid mwishoni mwa msimu huu, ambapo sasa anamalizia mkataba wake katika klabu ya Liverpool nchini England. 

Mbali ya beki huyo w akulia, wapo baadhi ya wachezaji wanatarajiwa kujiunga na klabu hiyo ikiwa na maana uamuzi umefanyika nani asajiliwe na nani aondoke ili kuwapisha wachezaji wapya. Real Madrid ipo katika nafasi ya pili ya Ligi Kuu Hispania kwa tofauti ya pointi 7 dhidi ya vinara Barcelona.

LUKA MODRIC

Nahodha huyu ni miongoni mwa nyota ambao wanatarajiwa kuondoka klabuni hapo. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, Real Madrid imeripotiwa kwamba imefanya uamuzi wa kutompa mkataba mpya na hivyo atakuwa miongoni mwa wanaoagwa kikosini hapo ili kupisha damu changa ambazo zitaongeza chachu ya ushini katika klabu hiyo. Akiwa na Real Madrid nyota huyo tangu alipojiunga akitoke Tottenham Hotspurs ametwaa mataji kama La liga, Cope Del Rey, Supercup, 

Ligi ya Mabingwa na klabu bingwa dunia. Kiungo huyo kutoka Croatia ana umri wa miaka 39, msimu huu amecheza mechi 29 za La liga, ambapo mechi 13 ameanza kwenye kikosi cha kwanza. Hata hivyo Modric anaelekea kumaliza kipindi chake cha uchezaji katika klabu ya Real Madrid. Nyota huyo alijiunga Real Madrid mwaka 2012 na tangu hapo amecheza mechi 583 klabuni hapo na ammefunga mabao 43 na kutengeneza 93. Ametwaa mataji 6 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mataji manne ya La Liga na mawili ya Cope Del Rey. Modric amedumu Real Madrid kwa miaka 13.

LUCAS VAZQUEZ

Winga huyo ambaye amegeuzwa kuwa beki wa kulia ni miongoni mwa wachezaji ambao wanatarajiwa kuondoka klabuni hapo. Lucas ni zao la Akademi ya Real Madrid, Castilla. Ujio wa Trent Alexandre Arnold una maana Lucas Vazquez anatakiwa kupisha nafasi hiyo. 

Lucas ana umri wa miaka 33 na anatarajiwa kutimiza mechi 400 akiwa Real Madrid. Kwa misimu mitatu mfululizo amechezeshwa kama beki wa kulia na mwanzilishi wa hilo ni Zinedine Zidane. 

Tangu wakati wa Zidane Lucas alikuwa akipangwa winga wa kulia au beki wa kulia. mara nyingi akicheza beki w akulia ilikuwa kuziba pengo la beki wao Dani Carvajal. Dani anauguza majeraha aliyopata mwanzoni mwa msimu huu na anategemewa kurudi uwanjani msimu ujao 2025/2026. Wakati Trent Alexandre Arnold akiwa chaguo la kwanza, mchezaji wa pili anayewindwa na Real Madrid ni kiungo Martin Zubimendi wa Real Sociedad na beki wa kati Dean Huijesen.

DAVID ALABA

Beki huyu anategemewa kuondoka klabuni hapo baada ya umri kumtupa mkono. Sababu nyingine ni majeraha ya mara kwa mara ambayo yamemweka kando. Nyota mwenye uwezo wa kucheza beki wa kati na kushoto alijiunga Real Madrid bure baada ya kumaliza mkataba wake Bayern Munich. Yeye ni kati ya wachezaji wenye umri mkubwa ambao wanategemewa kuachwa na Real Madrid ili kupisha damu changa. 

Katika nafasi ya beki wa kati anakabiliwa na changamoto kutoka kwa Raul Asencio, chipukizi kutoka Castilla aliyepandishwa hadi timu ya wakubwa baada ya mzigo wa majeruhi kuiandama Real Madrid. Katika nafasi ya beki w akushoto, David Alaba anakabiliwa na ushindani kutoka kwa Fran Garcia na Ferland Mendy, lakini uwezekano wa kuondoka ni mkubwa.

JESUS VALLEJO

Beki huyu wa kati amekuwa msugua benchi mzuri kwani hajapata nafasi ya kuwakilisha Real Madrid msimu huu. Takwimu zinaonesha amecheza mechi 1 msimu huu hali ambayo inamuwia vigumu kubaki klabuni hapo. Vallejo ana uwezo wa kucheza nafasi ya beki wa kati na kulia, lakini ushindani kutoka kwa Antonio Rudiger, David Alaba, Raul Asencio na Eder Militao umesababisha asugue benchi kwa muda mrefu. Ushindani mwingine unatoka kwa Jacobo ambaye amekuwa akiitwa mara kwa mara katika kikosi cha wakubwa akitokea Castilla.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version