Real Madrid bado kwa Atletico
*Juventus wawashinda Monaco
Real Madrid bado hawajapata dawa ya kuwanyoa wapinzani wao wa jadi, Atletico Madrid katika siku za karibuni.
Timu hizo zimekwenda sare kwenye mechi ya mkondo wa kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL).
Wakicheza ugenini, Real walibanwa ambapo mshambuliaji ghali zaidi duniani, Gareth Bale alizuiwa na kipa Jan Oblak kufunga alipopata nafasi ya mapema.
Mshindi atakayeingia nusu fainali atapatikana kwenye mechi ya marudiano itakayopigwa Santiago Bernabeu nyumbani kwa Real Aprili 22.
Kwenye mechi ya Jumanne hii, kipa wa Real, Iker
Vijana wa Carlo Ancelotti ambao ni mabingwa watetezi wanatafuta jinsi ya kuweka historia ya kushinda kombe hilo mfululizo kwa mara ya kwanza tangu AC Milan walipofanya hivyo 1989 na 1990.
Real walitwaa ubingwa huo mwaka jana kwa kuwachapa Atletico.
Real hawajawafunga Atletico tangu walipotwaa ubingwa huo wa Ulaya mwaka jana, ukiwa ni ubingwa wa 10, ambayo pia ni historia.
Real walichezesha moja ya jopo la washambuliaji wakali zaidi – Cristiano Ronaldo, Karim Benzema na Bale aliyekosa mechi ya La Liga iliyopita kutokana na kuumia paja.
JUVENTUS WAWAPIGA Monaco
Juventus wameanza vyema kampeni zao za UCL katika mechi ya robo fainali mkondo wa kwanza kwa kuwashinda Monaco 1-0.
Wanatafuta nafasi ya kucheza nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu 2003. Walipata bao kwa njia ya penati kupitia kwa Arturo Vidal kwenye mechi waliyocheza nyumbani Turin.
Yannick Ferreira-Carrasco aliwakosesha wageni bao la wazi kabla ya Carlos Tevez wa Juve kucheza vibaya mpira aliotakiwa kuuelekeza nyavuni.
Vidal alifunga penati iliyotolewa baada ya Ricardo Carvalho kumchezea vibaya Alvaro Morata. Kocha wa Monaco, Leonardo Jardim alilalamika kwamba matokeo hayo si ya haki kwa madai kwamba penati iliyotolewa haikustahili kwa madai rafu ilifanyika nje ya eneo husika.
Kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri ameeleza kufurahia matokeo, hasa kwa kutoruhusu bao nyumbani, akisema ni faida kidogo kwao kwenye mchezo wa marudiano.