*PSPF YATOA MSAADA WA MAGODORO UDSM, BAADA YA AJALI YA MOTO*
*Yatoa magodoro 118*
MFUKO wa Pensheni wa PSPF, leo Agosti 24, 2015, umekipatia Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, UDSM, magodoro 118 ili kusaidia huduma ya malazi kwa wanachuo walioathirika kutokana na bweni lao kuungua moto kwenye hosteli ya chuo hicho Mabibo jijini Dar es Salaam Aprili mwaka huu.
Akikabidhi msaada huo kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, (Anayeshughulikia masuala ya Utawala), Profesa David A. Mfinanga, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, amesema, PSPF, iliguswa na ajali hiyo ya moto ambayo iliyotokea kwenye bweni kitalu namba B na kusababisha mamia ya wanachuo kupoteza mali zao.
“Kwa kutambua kuwa wanachuo ni sehemu ya jamii ya Watanzania, na pia ni wanachama watarajiwa wa Mfuko, tumeona tuchangia sehemu ya vifaa ili wanafunzi waweze kurejean katika hali yao ya kawaida.” Alisema Njaidi.
Akitoa shukrani zake, kwa niaba ya Chuo, Profesa Mfinanga aliishukuru PSPF, kwa msaada huo ambao kwa hakika umesaidia pakubwa, kwani magodoro hayo yatapelekwa kwa walengwa na hivyo kusaidia kuwapunguzia machungu waliyoyapata kutokana na kuunguliwa vifaa vyao.
Kwa mujibu wa viongozi wa Chuo hicho, jingo hilo lilikuwa ,linakaliwa na wanachuo 788, wakati linawaka moto.