in

PSPF, BENKI YA POSTA, PROPERTY INT LTD, KWA PAMOJA WAZINDUA…

Leo Agosti 18, 2015 Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania na Taasisi ya Property International Ltd wamezindua mpango maalum wa kutoa mikopo ya viwanja kwa wanachama wa mfuko huo.

Lengo la mkopo huu wa viwanja ili kuwawezesha wanachama wa mfuko huu kumiliki viwanja vilivyopimwa na vilivyo halali kwa mujibu wa taratibu za nchi. Nia ni kwenda sambamba na dira ya PSPF ambayo ni kutoa huduma bora zenye ushindani katika sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa wateja wa PSPF.

Na pia kuitikia mwito wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), walioagiza Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii kutoa mafao kwa fomula iliyo sawa kwa watumishi wote. Hivyo kuanzia wakati huo Mifuko ya Hifadhi inapaswa kushindana kwa ubora wa huduma na vivutio vingine kwa wananchama na wananchama watarajiwa.

Ni dhahiri kuwa kila Mtanzania anahitaji kuwa na makazi bora ya kudumu, hivyo mpango huu unaozinduliwa leo hii ni mpango mzuri sana hasa kwa Watanzania wengi ambao hawana uwezo wa kutoa fedha taslimu. Utaratibuu huu wa kuwakopesha utawanufaisha wengi na hatimaye kufikia kauli mbiu ya Serekali yetu ya kuhakikisha Maisha bora kwa kila Mtanzania.

Mfuko wa Penshini wa PSPF umeendeleza ushirikiano wake mzuri na Benki ya Posta Tanzania, ambapo kama mnavyofahamu ushirikiano wao ulianzia kwenye utoaji wa Mikopo kwa Wastaafu, Mkopo wa Elimu na Mkopo wa kuanzia Maisha kwa wanachama wapya. Jitihada hizi zote ni katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wanachama wake, na pia katika kuonesha imani kwa Benki ya Posta, ambayo huduma zake bora zinapatikana kote nchini. Mahusiano haya na Property International Ltd yanazidi kujenga mahusiano haya kwa maslahi ya wanachama na Watanzania kwa ujumla.

Wanachama wa PSPF waliochangia Mfuko kwa kipindi kisichopungua miezi sita wanasifa zote za kuweza kukopa viwanja hivi, na watapaswa kulipa ndani ya miaka mitatu. Wanachama walio katika mpango wa Uchangiaji wa Hiari pia watafaidika na mkopo huu. Wanachama wote wa Mfuko wa Hifadhi wa PSPF wanakaribishwa sana kupata mkopo huu maalum kwa ajili yao.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

BAO LA BENTEKE HALIKUWA BAO HALALI

Chelsea wawapandia Man U