Menu
in , , ,

PSG watema £88m kumtwaa Ronaldo

*Iker Casillas: Mleteni De Gea, mleteni haraka
*Khedira: Ni huru, natoka Madrid kwa simanzi
*Man City wamtaka Sterling, Liver ni Benteke

Paris Saint-Germain wamewapiga kumbo Manchester United katika mbio za kumuwania Cristiano Ronaldo wa Real Madrid kwa kutangaza dau la pauni milioni 88 ili kumpeleka nyota huyu Mreno Ufaransa.

Ronaldo, 30, hajapata kuonesha nia ya kuondoka Madrid, licha ya Man United kuonesha heshima kwake naye pia kuwaonesha hivyo, hasa anapocheza dhidi yao, ambapo pia huwa hashangilii bao dhidi yao. Hakuondoka Old Trafford kwa ugomvi.

PSG wanataka kuonesha jeuri ya fedha, ambapo baada ya kutwaa ubingwa wa Ufaransa wangependa kuona wachezaji wa hali ya juu wakiwa kwao. Man United wamepata kufikiria kumrejesha mchezaji huyo, lakini haitarajiwi watatoa dau kubwa hivyo. Kubwa zaidi walilopata kutoa ni pauni milioni 59 kwa Angel Di Maria aliyeoka Real mwaka jana.

Wafaransa hao pia wameanzisha mchakato wa kutaka kumchukua kiungo wa United aliyehamia huko kutoka Real na kushindwa kuwika msimu huu, Angel Di Maria, 27, wakitaka kumsajili kwa mkataba wa mkopo kwa msimu mmoja.

Golikipa wa Real Madrid, Iker Casillas, 34, amewaambia waajiri wake wasiwe na kigugumizi cha kumsajili kipa namba moja wa Manchester United, David De Gea, 24, hata kama kwa kufanya hivyo atamchukulia nafasi yake ya kwanza kwenye timu.

Manchester United wamepewa ofa ya kipa kutoka Costa Rica, Keylor Navas, 28, akiwa kama chambo ya kumvutia De Gea hadi Real Madrid. De Gea ni raia wa Hispania aliyezaliwa Madrid na kucheza Atletico Madrid kabla ya kwenda Old Trafford.

Kiungo wa Real Madrid, Sami Khedira, 28, amewaaga wachezaji wenzake, akisema kwamba ilikuwa mara yake ya mwisho kuwa kwenye mazoezi na timu anayoipenda sana.

Khedira aliyekuwa akiwindwa na Arsenal msimu uliopita, amesema kwamba amesikitishwa na uamuzi wa baadhi ya wakubwa wa Real Madrid kutomtaka kwenye timu kiasi cha kuzuia asichezeshwe kwenye mechi nyingi zilizopita.

Mchezaji huyu wa kimataifa wa Ujerumani amesema kwamba madai yaliyokuwa yakitolewa kwamba alikuwa na majeraha na asingeweza kucheza si kweli, kwani alipata jeraha dogo sana la goti, aina ambayo wachezaji wengine huendelea nayo dimbani bila tatizo.

Tangazo hilo ni king’ora kwa klabu za Ligi Kuu ya England zitakazomtaka kwani baada ya mwezi mmoja atakuwa mchezaji huru.

Wakati Manchester City wakiamua kuingia kwenye vita ya kumsajili mshambuliaji wa Liverpool, Raheem Sterling na kuwa tayari kutoa pauni milioni 45, inadaiwa Liverpool wanaanza kulainika, lakini sasa wanasema watapenda walipwe pauni milioni 60 na majadilianoyakifanyika wanaeza kushuka hadi juu kidogo ya pauni milioni 50.

Liverpool walifutilia mbali majadiliano ya mkataba mpya na Sterling Ijumaa hii baada ya wakala wake kusema ‘mbovu’ akidai kwamba Sterling anabaki na msimamo wake wa kutosaini mkataba mpya hata kama wangeamua kumlipa pauni milioni 900 kwa wiki.

Ikiwa Sterling atauzwa kwa zaidi ya pauni milioni 50, Queen Park Rangers (QPR) watapewa mgawo wa pauni milioni 10 kwa sababu alicheza huko tangu 2003 hadi 2010 Liverpool walipomnunua.

Chelsea na Arsenal nao wanadaiwa pia kumtaka mzaliwa huyo wa Jamaica mwenye umri wamiaka 20, lakini Man City tayari wamepeleka barua kwa Liverpool kumtaka mchezaji huyo. Sterling hakupangwa katika kikosi cha 11 wa kuanza mechi ya mwisho ya msimu.

Liverpool wameanza kuangaza huku na kule ili kuziba pengo tarajiwa la Sterling. Inasemekana wanamwinda mshambuliaji wa Aston Villa kutoka Ubelgiji, Christian Benteke, 24, na mkononi wanazopauni milioni 30.

Hata hivyo, kocha wa Aston Villa, Tim Sherwood anaamini kwamba Benteke anataka kubaki Villa Park msimu ujao. Kadhalika anachuana na Liverpool na Newcastle kumsajili mlinzi wa Manchester City,

Micah Richards, 26, ambaye mkataba wake unamalizika kiangazi hiki.
Liverpool, hata hivyo, wanaweza kupata matumaini kwa sababu inaelekea kiungo wa Manchester City, James Milner, 29, atajiunga nao na si Arsenal waliokuwa wametajwa awali.

Kocha wa muda wa Sunderland, Dick Advocaat, 76, atapanda ndege Jumatatu hii hadi kwao Uholanzi kumuomba mkewe amruhusu abakie na klabu hiyo kwa miezi 12 zaidi. Alikuwa ameruhusiwa kwa miezi mitatu tu kuwanusuru klabu kushuka daraja, jambo alilofaulu. Mkewe hapendi Advocaat akae ng’ambo muda mrefu.

Mshambuliaji wa Hull, Nikica Jelavic, 29, atatafuta klabu ya Ligi Kuu ili ahamie kwa mkopo ikiwa Hull watashuka daraja. Arsene Wenger amepanga tarehe ya kufanya kikao kigumu na mchezaji wake aliyebakisha mwaka kwenye mkataba, Theo Walcott, 26.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Exit mobile version