ZAMA za kazi ya Paul Pogba katika soka zaweza kuwa zimefikia ukingoni, baada ya kuadhibiwakutojihusisha na shughuli za michezo kwa miaka mine, ikionekana kwamba kiungo huyu wa Juventusmwenye umri wa miaka 30 hakutumia vyema muda na nguvu zake.
Mchezaji huyu wa zamani wa Manchester United, aliyetwaa Kombe la Dunia akiwa na Ufaransa, alionekana Dhahiri kuwa mtu mwenye kipaji kikubwa akionekana ni nyota wa dunia, lakini ikatokea kwamba hakuonesha hayokwa uendelevu.
Tayari amesema kwamba atakata rufaa kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), lakini huko akishindwa tena, itamaanisha kwamba katika muda ambao ataruhusiwa kurejea tena dimbani – Agosti 2027 – atakuwana umri wa miaka 34, akiwa hana klabu, pengine pasipo mazoezi yanayotakiwa na ari ya kucheza tena.
Kwa hiyo utakuwa ni mtihani mkubwa kwa mchezaji ambaye hajapata kuweza kucheza usawwa wa mechi 22 za ligi kwa msimu tangu 2018/19 kubaki na utimamu wa mwili na kuwa na hamasa ya mazoezi kwa kipindi kirefu kama hiki alichopewa.
Mwandishi wa michezo wa Ufaransa, Julien Laurens, alisema katika BBC Radio 5 Live’s Euro Leagues Show: “Nakumbuka nikimwona akiwa kama na umri wa miaka 15 na alikuwa kifaa bora Zaidi nilichopata kuona, alikuwa mzuri, kipaji kikubwa cha kizazi chake na mwenye akili na ufundi wa ajabu uwanjani.
“Alikuwa na wakati mzuri mchezoni, alishiriki na timu kutwaa bingwa wa Ligi Kuu ya Italia – Serie A- mara nne na Kombe la Dunia kadhalika. Ni wakati mzuri sana huo. Hakika alikuwa mtamu hadi nikawaza kwamba hapangekuwa na kizzuizi cha mwisho kwake.
“Nilidhani angepanda na kufika kileleni kabisa n ahata kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia ‘Ballons d’Or’, au kwamba angeshinda makombe Zaidi na kuw amchezaji bora zaidi duniani. Mwishowe tutabaki kutazama nyuma kwenye enzi zake, pengine naye pia akiwaza kipialitakiwa kufanya.
Pogba alisimamishwa kucsoka kwa muda Septemba baada ya vipimo vya kutumia dawa za kuongeza nguvu kuonesha alifanmya hivyo. Baraza linalopambana na dawah hizo nchini Italia – Nado) lilithibitisha kmfungia kwa miaka mine, na adhabu hiyo inaanzia nyuma, ikimaanisha Agosti mwaka 2023 alipopimwa.
Pogba alidai kwamba hukumu hiyo haikuwa sahih na kwamba hajawahi wala hatakaa, akijua, kutumia dawa hizo. Alithibitiosha kwamba angekata rufaa na kuongeza kwamba atakapokuwa hurudhidi ya vizingiti vya kisheria, simulizi kamili litatoka kwa undani wake.
Pogba alizaliwa Lagny-sur-Marne, akajiunga na timu ya vijana ya Daraja la Pili Italia, Le Havre 2007, kabla ya uhamisho wenye utata kwenda Manchester United miaka miwili baadaye. Tena, miaka miwili baadaye, kutokana na kukosa nafasi zakucheza mara kwa mara, Pogba aliondoka na kujiunga na Timu ya Ligi Kuu ya Italia, Juventus akiw mchezaji huru.
Alisaidia klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Serie A mara nne mfululizo, lakini pia wakatwaa Coppa Italia mara moja na Supercoppa Italiana mara mbili. Alijijenga na kutokea kuwa mmoja wa wachezaji wanaoibukia wenye kutia matumaini makubwa duniani, na alitwaa kiatu cha dhahabu 2013kikifuatiwa na Tuzo ya Bravo mwaka2014. Ilipofika mwaka 2016 Pogba alitajwa kwenye timu ya wachezaji bora wa UEFA.