*Nenda Mwamba, tutakufuata
DUNIA inasikitika kutokana na kifo cha mwanasoka mahiri wa siku zote, Edson Arantes do Nascimento, aliyejulikana zaidi kwa jina la Pele aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.
Mwanaume huyu aliyetokea kuwa nyota wa kwanza mkubwa wa soka duniani, alifanyiwa upasuaji kutokana na maradhi ya saratani Septemba mwaka jana, kasha akawa anapatiwa matibabu na uangalizi wa karibu nchini Brazil.
Mastaa wa soka duniani wameandika ujumbe kupitia akaunti zao Instagram na Twitter, wakionyesha jinsi ganni wameguswa a kifo cha mkongwe huyo aliywahi kujipatia umaarufu kutokana na kipaji chake cha soka.Alikuwa sehemu ya kikosi cha Brazil kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 1958, 1962 na 1970 na bado anashikilia rekodi ya kuwa mwanasoka mdogo zaidi kupata kushinda kombe hilo kubwa zaidi duniani.
David Beckham Mkongwe wa soka aliyewahi kukipiga Manchester United na Real Madrid aliandika “Asante ‘Pele’ hakika alikuwa na kipaji cha kucheza soka”, naye Ronaldo de Lima, Rorbeto Carlos, Gary Lineker, Sir Geoff Hurst, miongoni waliondika ujumbe kuhusu kifo cha Pele.
Pele aliupa mchezo huo sifa, pale alipokuja na msemo kwamba ‘soka ni mchezo mzuri’, na anachukuliwa kwamba ndiye mwanasoka aliyeucheza vyema zaidi na kwa furaha, kiasi cha kuitwa ‘Mfalme’ huko kwao Brazil. Anachukuliwa kuwa bora zaidi, huku wengine wakitajwa kuwa ni Pelé Diego Maradona, Lionel Messi, Johan Cruyff na Cristiano Ronaldo.
Alikuwa mwanasoka mwenye nguvu kubwa na kasi, akiwachambua na kuwapeleka puta mabeki na alikuwa na nguvu ya aina yake katika kupiga mipira na kupachika mabao, na aliweza kufunga kutoka kwenye kona ambazo mtu angedhani haiwezekani kufunga.
Alikuwa na uwezo mkubwa wa mipira ya juu, japokuwa alikuwa na urefu wa futi 5.9, akitumia misuli yake yenye nguvu ya shingo kuhakikisha mpira unakwenda anakotaka, kama alivyofanya alipofunga bao la kwanza kwenye la Kombe la Dunia 1970 dhidi ya Italia.
“Nahisi maarifa makubwa niliyo nayo kwenye uwanja wa soka ni kufanya kitu kutoka kusiko na kitu,” alisema.
Hivi ni viwango vilivyompelekea Pele kuwa na mabao kiasi cha 1,281 (namba halisi ina ubishani) kwenye mechi 1,363 alizocheza kati ya 1956 na 1978. Alifunga mabao 77 kwneye mechi 92 za Timu ya Taifa ya Brazil na mabao 1,090 katika mechi 1,114 akiwa na klabu yake ya Santos ya Brazil.
Alizaliwa kwenye kijiji cha wachimba madini cha Tres Coracoes katika jimbo la Minas Gerais. Alipewa jina hilo la utani la Pele shuleni, lakini hajui kwa nini. Baba yake, Dondinho, naye alikuwa mwanasoka miaka ya ’40. Ndoto yake ya kwanza ilikuwa kuwa rubani wa ndege, lakini mapema ikaonekana kwamba mwelekeo wake ni kwenye soka.