Menu
in , , , ,

Nyota wa EPL watakaokuwa AFCON

*AFCON yaipokonya EPL nyota wake

Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zinakaribia, huku kwenye Ligi Kuu ya England (EPL), watu wakiangalia nani atakosa mechi kwa sababu ya kuwa nyumbani Afrika kupeperusha bendera ya taifa lake.

Hapana shaka kwamba kiungo wa Manchester City, Yaya Toure ndilo jina kubwa miongoni mwa wachezaji 19 wa EPL watakaoikosa ligi hiyo kwa ajili ya kucheza kwenye AFCON na wengine kwenye Kombe la Asia.

Iwapo Ivory Coast itasonga mbele hadi hatua ya fainali Februari 8, basi Toure atakosa walau mechi tano, ikiwamo dhidi ya vinara wa ligi wa sasa, Chelsea, itakayopigwa Januari 31.
Hata hivyo, Toure ambaye ni mchezaji bora wa Afrika, anaweza kuwapo kwa ajili ya safari ya kwenda Stamford Bridge iwapo The Elephants hawatavuka hadi hatua ya fainali. Toure ni mtu muhimu kwa City, maana amekuwa kama injini yao.

AFCON inaanza Jumamosi hii wakati michuano ya Asia itakayochukua wiki tatu inaanza Ijumaa hii, ambapo klabu 12 kati ya 20 za EPL zitakosa huduma za wachezaji kadha.
Wanaoathiriwa zaidi na kutokuwapo kwa wachezaji hao ni pamoja na Southampton ambao wanafukuzia sana nafasi za juu za ligi, kwani hawatakuwa na wachezaji watatu wa kikosi cha kwanza sawa na walivyo Crystal Palace wanaopigana kuepuka kushuka daraja.

Palace wataendeleza vita yao kuwania kubaki juu wakiwa hawana wachezaji Yannick Bolasie wa Kongo Kinshasa, Adlene Guedioura wa Algeria na Mile Jedinak wa Australia. Hao wamecheza zaidi ya dakika 1,600 kwenye soka ya daraja la juu kabisa msimu huu.

Klabu hizo zinaweza pia kuwakosa wachezaji hao kwenye michuano ya Kombe la FA na Kombe la Ligi, kutegemeana na ni kwa muda gani mataifa yao yatakuwa yakisonga mbele kwenye michuano ya AFCON.

Everton watawakosa Christian Atsu wa Ghana, Leicester hawatakuwa na Riyad Mahrez wa Algeria wakati Liverpool watakosa huduma za Kolo Toure wa Ivory Coast. Newcastle United hawatakuwa na Papiss Cisse wa Senegal wala Cheick Tiote wa Ivory Coast.

Southampton pigo lao ni kutokana na Sadio Mane (Senegal), Emmanuel Mayuka (Zambia) na Maya Yoshida wa Japan) kuwa na timu za mataifa yao huku Stoke wakimkosa Mame Biram Diouf wa Senegal. Hata hivyo, Mane kwa sasa ni majeruhi, ila kocha wa Senegal, Alain Giresse amesema anafuatilia hali yake na wakati wowote atakuwa naye kikosini, licha ya kocha wa Southampton, Ronald Koeman akisisitiza kwamba hawezi kucheza.

Swansea (au kwa sasa tuseme Manchester City) hawatakuwa na Wilfried Bonny anayekuwa Afrika baada ya kuhitimisha dili la usajili kwa pauni milioni 28 kutoka Swansea kwenda City, lakini pia michuano ya Asia inawapokonya Ki Sung-yueng wa Korea Kusini.
Tottenham Hotspur wao hawatakuwa na Banil Bentaleb wa Algeria huku West Bromwich Albion wakmkosa Youssouf Mulumbu wa Kongo Kinshasa.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version