Menu
in

Nini kimewatokea TP Mazembe?

TP Mazembe

TP Mazembe

KATI ya timu 16 zilizoshiriki mashindano ya Shirikisho la soka barani Afrika, Mabingwa wa zamani wa Ligi ya Mabingwa TP Mazembe wameambulia pointi mbili.

Wakati mabingwa wa soka nchini Tanzania Simba wakiwa wanashika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 13 walizojikusanyia kutoka kundi A sambamba na vinara wa pointi hizo Mamelodi Sundowns, lakini hali ya vijana wa Moise Katumbi ni mbaya zaidi.

Kwenye mchezo wao dhidi ya Mamelodi Sundwons ilishangaza kuona TP Mazembe ikigeuzwa geuzwa kama chapatti. TP Mazembe ilichezewa mpira wa kiwango cha juu na hakika lilikuwa jambo la kushangaza.

Namna TP Mazembe ilivyofanyiwa dhihaka kiuchezaji na Mamelodi ilikuwa ujumbe tosha kwa mtu anaytafakari kujiuliza nini kimetokea kwa miamba hiyo ya soka kutoka DR Congo?

TP Mazembe imetupwa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa kwa aibu baada ya kushindwa kufuzu hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008.

Ikumbukwe TP Mazembe ni mabingwa mara tano wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika. Ni mojawpao ya klabu kongwe na tishio linapokuja suala la mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mbaya zaidi, TP Mazembe ilikubali kipigo cha mabao 2-0 na Belouizdad ya Algeria kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B hivyo kuondolewa mashindanoni.  Kabla ya mchezo huo TP Mazembe ilichapwa mabao 2-1 na vinara wa kundi B, Mamelodi Sundwons ya Afrika kusini.

Vipigo walivyopata msimu huu vimeharibu rekodi yao ya kutofungwa mechi 74. Kabla ya hapo mara ya mwisho TP Mazembe kupoteza mchi ya nyumbani ya CAF ilikuwa Oktoba mwaka 2009, ambapo ilizabwa mabao 2-0 na Al Hilal ya Sudan katika mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Washabiki wengi wanajiuliza ni kitu gani kimetokea kwa miamba hiyo ya soka Afrika? Kama suala la uwekezaji basi TP Mazembe kiwango chao ni cha juu kuanzia aina ya wachezaji wanaowasajili kwa gharama kubwa,bajeti ya uendeshaji wa timu,mishahara,bonasi na mengineyo si mambo yanayowasumbua.

Zipo klabu barani Afrika zikiwa na changamoto ya kuwalipa wachezaji wao hadi kufikishana FIFA kwa mashtaka na usuluhishi ili haki itendeke, lakini kwa TP Mazembe ni timu kubwa.

Hii ndiyo timu ambayo ilimuuza Mbwana  Samatta kwenbda Genk ya Ubelgiji ikiwa inatazamwa kama kisima cha kuibua nyota wenye vipaji. Kwahiyo sifa zake hazitarajiwi kuona wakishindwa kufuzu hatua ya robo fainali.

Ligi ya DR Congo inaendelea, huku TP Mazembe wanaongoza baada ya kujikusanyia pointi 43 mbele ya F.C Lupopo. Hiyo ina maana washabiki walitarajia TP Mazembe kuonesha kiwango kikubwa cha kusakata kandanda kwenye Ligi ya Mabingwa. Limekuwa jambo la aibu kushuhudia wakongwe hao wakiambulia pointi mbili katika kundi B.

Takwimu za CAF zinaonesha kuwa timu ya tatu ni Waydad Casablanca,Mamelodi Sundowns na Simba ndizo zimefanya vizuri zaidi kuliko zingine kwenye mashindano ya CAF msimu huu.

Baada ya hapo zinafutiwa na timu zenye wastani wa kawaida kimafanikio msimu huu zikiwemo Esperance, A Ahly, Horoya,MC Alger,Kaizer Chiefs, CR Belouizdad,Zamalek,Teugheth, A Hilal,AS Vita, Al Marreikh na Petro De Luanda.

Kwenye kundi A, klabu ya AS Vita DR Congo imeshika nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Al Ahly ya Misri. Hakuna aliyetegemea kuwa Simba ingeongoza kundi hilo, lakini yote yamebaki historia. Wakati AS Vita ikiwa imepitwa na TP Mazembe kwenye ligi ya DR Congo lakini angalau imevuna pointi katika kundi A na kuficha aibu ya Wakongomani kwenye mashindano ya CAF.

Kwa upande mwingine wa soka, ni wakati ambao timu za nyumbani Tanzania zinatakiwa kujifunza mpira wa miguu ulivyo, licha ya uwekezaji mkubwa bado timu inaweza kufanya vibaya na kushangaza zaidi. hapo ndipo unakutana na timu kama Belouizdad nazo zinajiokotea pointi kwa TP Mazembe.

Mashabiki wanatakiwa kujua kuwa wakati mwingine timu inafeli kwa sababu haina uwezo, bali inakumbana na msimu mbaya na kuikosesha mataji mbalimbali.

Pengine baada ya kutolewa Ligi ya mabingwa, TP Mazembe itaelekeza nguvu zake kwenye Ligi ya ndani, lakini hiyo si kigezo cha timu hiyo kufanya vizuri msimu ujao ikiwa watacheza mpira mbovu kama walivyofanya msimu huu kwenye Ligi ya Mabingwa.  

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version