Menu
in , , , ,

NINAVYOMFAHAMU ERASTO ZAMBI

Nikiwa njiani kutoka Morogoro kulikokuwa kukifanyika mashindano yaTaifa  kutafuta  klabu bingwa nchini   mpira wa wavu napokea simu kutoka  kwa Mwinga Mwanjala Afisa Utawala wa   Kamati ya Olimpiki Tanzania  akinieleza rafiki yako Erasto Zambi  hatuko naye tena amefariki  usiku wa leo.

Ukweli nilihuzunika sana kwa taarifa ile. Kilichohuzunisha zaidi ni yale masihara niliyokuwa nikimtania kila tukikutana. Ni siri gani waliyokuwa nayo kwani toka waondoke  hatujaambulia hata medali ya  bati . Ni miaka 32 sasa kuna nini. Kwa masihara naye alipenda kusema hamtaki kuja kuniona . Wazee tunaondoka hamtaki kuja kufahamu siri.

Erasto Zambi ana historia ndefu kimichezo kwani alitumia zaidi ya  nusu ya maisha yake  katika michezo.

Miongoni  mwa wanafunzi wake  kimichezo ni pamoja  na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa  Tanzania  Jakaya Mrisho  Kikwete katika mchezo wa Basketball.Zambi alipenda sana kusema kuwa Kikwete alikuwa mwanafunzi wake bora  kwani hata walipokuja walimu na wachezaji bora wa Marekani kama vile Kareem Al Jabaar walimsifu sana  Jakaya.

Erasto Zambi alizaliwa mwaka 1938 mkoani Mbeya.  Akiwa mwalimu wa michezo aliajiriwa na Shirika la Elimu Kibaha mapema miaka ya sitini.  Shirika la Elimu Kibaha ndio Shirika pekee wakati ule  la msaada toka nchi masikini za Scandanavia wakati ule kwenda kwa nchi masikini  Afrika kwa maendeleo.

Sina hakika Shirika la Elimu Kibaha lilienziwa vipi katika miaka hamsini ya Uhuru wa Tanganyika

Hata hivyo mapema miaka ya sabini Erasto Zambi  alijikuta akiajiriwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM kama mwalimu wa michezo hapo chuoni. Wanafunzi wengi waliopitia hapo chuoni akiwemo Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF Leodgar Tenga wamepitia katika mikono yake.

Binafsi kamwe sitomsahau kwa kunifungua macho katika ulimwengu wa michezo. Alikuwa ni Erasto Zambi aliyehakikisha Tanzania inakuwa mwanachama wa Shirikisho la Mpira wa Wavu Duniani  FIVB mapema miaka ya themanini Tanzania ilijiunga na Shirikisho la Mpira wa Wavu FIVB  1984.

Zambi alitoa kila aina ya msaada ikiwemo kulipa ada  kwa Shirikisho hilo kuhakikisha Chama cha Mpira wa Wavu nchini TAVA  kinapata utambulisho wa kimataifa. Kama vile haitoshi Zambi alitoa msaada mkubwa kwangu kwa kuhudhuria mafunzo mbali mbali  ya uongozi wa michezo kupitia Kamati ya Olimpiki Kimataifa International Olympic Committee kule Olympia Greece mwaka 1984.

Alipenda sana nijifunze mengi kiuongozi wakati ule

Zambi alinishirikisha pia katika mafunzo ya kwanza nchini mwaka 1997 kutafuta Wakurugenzi wa mafunzo ya Utawala wa michezo  Sports Administration chini ya Kamati ya Olimpiki Duniani.

Watanzania wawili  ikiwa  pamoja na Ndugu Samson Kayobyo tulibahatika kufanikiwa kufaulu mafunzo hayo. Ingawa leo Tanzania ina watu zaidi ya kumi kwenye Tanzania Olympic Academy bado Erasto Zambi ana mchango mkubwa  unaohitaji kuenziwakatika uanzilishi wa Academy hiyo.

Mchume mimi nimetembelea karibu nchi zote Duniani alipenda kusema mara nyingi tunapokutana .

Ni kweli sina ubishi na hilo kwani amekuwa  Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki  Tanzania  kwa karibu miaka 27.

Naamini wanamichezo kwa ujumla tutafuata yale yote mema alioyatenda  na kumuenzi .

Mungu ailaze roho ya marehemu Zambi  mahali pema peponi.

Makala hii imeandikwa na Muharame Mchume

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version