Menu
in , , ,

Nililia machozi kwa kuchukuliwa Mbuyu Twite, Ilikuwa rafu moja mbaya sana-Rage

 

Hivi karibuni nilikutana na kiongozi wa timu ya Simba na Mbunge wa Tabora mjini, Mhe Ismail Aden Rage, jijini London, haya ni maswali niliyomuuliza, naye kuyatolea majibu katika sauti:(nasikitika kwa ubora hafifu wa sauti):

1. Bwana Rage una historia ndefu na klabu ya Simba tangu mchezaji mpaka kiongozi wa nafasi tofauti. Hebu tueleze kwa ufupi historia yako ndani ya klabu hiyo.

2. Katika kuweko kwako kote ndani ya Simba ni wakati gani ulishiriki kuipa klabu hiyo mafanikio makubwa kuliko wakati mwingine ukiwemo ndani ya klabu hiyo kama mchezaji, Katibu Mkuu au Mwenyekiti?

3.Ukiwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba ni dhahiri kabisa umekuwa ukishindwa na Yanga kupata haki zako kuhusu umiliki wa wachezaji kama ulivyompoteza bure beki Kelvin Yondani, ulivyonyanga’anywa beki Mnyarwanda Mbuyu Twite na ulivyompoteza winga mwenye kasi Mrisho Ngassa. Unavyofahamika wewe ni muelewa na mchambuzi mzuri wa kanuni:-
a) Kwa nini hukuzingatia vizuri kanuni ili kufanikisha umiliki wa wachezaji hao dhidi ya watani wako wa jadi Yanga?
b) Kwa nini hukuchambua vizuri kanuni kuona Yanga ilikosea mahali katika kuwanyang’anya wachezaji hao?
c) Mbona katika kesi zote hizo ulionekana kuwa baridi sana tofauti na nguvu zako unapopigania haki, je kulikuwa na shinikizo lolote toka mahali fulani pazito?

4. Katika suala la Mbuyu Twite ulilia machozi ulipokuwa ukilieleza kwa waandishi wa habari. Nini hasa kilikuliza katika sakata lote hilo? Nini tafsiri ya machozi yako?

5. Hebu tueleze kuhusu biashara tata ya mchezaji wenu Emmanuel Okwi wa Uganda kwa Etoile du Sael  ya Tunisia. Mgogoro wa malipo uko vipi na unaamini FIFA wanaweza wakaamua vipi kuhusu suala hilo? Je mchezaji huyo anaweza kwenda Yanga kama inavyovumishwa sasa hivi? Ili aende klabu nyingine mbali ya Simba na Etole du Sael utaratibu wa kwenda huko utakuwaje?

6. Ulipoingia Simba kama Mwenyekiti mwaka 2010 uliahidi mambao kadhaa ambapo mawili makubwa ni kuhakikisha Simba Sports Club inanufaika na rasilimali zake kwenye mtaa wa Msimbazi yalipo makao makuu yake kwa kuhakikisha inakuwepo mikataba halali ya wapangaji kulingana na gharama halisi ya upangaji kwenye eneo hilo la Kariakoo na jingine ni mchakato wa ujenzi wa uwanja wa klabu ya Simba kule Bunju. Je mmefikia wapi kwa hayo yote mawili? Kama kuna mikwamo, nini sababu ya mikwamo hiyo?

7.Hivi karibuni ulionekana kwenye vyombo vya habari ukiwasainisha wachezaji wawili kuichezea klabu ya Simba, mmoja ni mtanzania kutoka Misri na mwingine toka Mtibwa Sugar. Nafahamu wewe ni mhasibu kitaaluma kama sijakosea lakini ulionekana ukiwasainisha wachezaji hao huku kiasi cha pesa kikiwa hapo mezani ikimaanisha ni malipo yao. Huu ni utaratibu sahihi wa kifedha badala ya kuwalipa kwa hundi? Je wachezaji hao ni pendekezo la kocha au ni mipango yako binafsi?

8. Simba kwa sasa ni wazi iko kwenye mgogoro baada ya wewe Mwenyekiti kusimamishwa na kamamti ya utendaji uenyekiti ukiwa nje ya nchi. Kwa mujibu wa katiba ya Simba, kamati ya utendaji ina mamlaka hayo? Kama inayo, katika mazingira yapi?

9. Kwa nini TFF ilipokuagiza uitishe mkutano mkuu wa dharura ndani ya wiki mbili kuzungumzia mgogoro huo, ulikaidi hadharani kwa kueleza kuwa hautatekeleza hilo? Umezingatia kanuni gani kukaidi agizo hilo na kwa nini msingewasiliana na TFF wenyewe tu badala ya kuumbuana hadharani kupitia vyombo vya habari?

10. Nani atakuwa kocha mkuu wa Simba kati ya Mtanzania King Abdallah Kibaden na Mkroatia Zdravko Logarusic ikizingatiwa kuna pande mbili kila moja ikimzungumzia mmoja wa makocha hao? Nani mwenye maamuzi ya kuajiri na kufukuza kazi kocha kwenye klabu ya Simba?

11. Una mkakati gani wa kumaliza mgogoro wa sasa wa Simba ili kurudisha umoja ndani ya klabu hiyo?

 

[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/125304283″ params=”color=ff6600&auto_play=false&show_artwork=true” width=”100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version