Menu
in , ,

NILICHOKIONA KWENYE MECHI YA BAYERN MUNICH NA ARSENAL

Tatizo la Arsenal ni lile lile la Msimu wote. Kushindwa kupigana
kwenye mechi kubwa, kukosa kiongozi sahihi wa mapambano kwa mechi
husika na mwisho wa siku timu kucheza kwenye hali ya Unyonge pindi
inapocheza mechi kubwa.

Jana kwa dakika 25 za Mwanzo Arsenal hawakuwa na uwezo wa kukaa na
mpira hata kwa zaidi ya sekunde 20.

Hili ni tatizo kubwa sana hasa hasa unapocheza na timu ambayo
inawachezaji wa kiwango cha juu, kwa sababu unapokutana na timu za
namna hii unatakiwa uhakikishe timu yako iwe na nafasi ya kumiliki
mpira pindi inapopata mpira.

Lakini hiki hakikuwepo kwa upande wa Arsenal. Kwa dakika hizo 25 za
mwanzo wachezaji walikuwa hawana uwezo wa kumiliki mpira hata kwa
sekunde 20 hata kuweza kupiga pasi kwa usahihi.

Inawezekana baada ya Arsenal kusawazisha goli, waliamini wanaweza
wakafunga tena, ndiyo maana walianza kufunguka kwenda mbele kufanya
mashambulizi.

Kitu ambacho kilikuja kuimaliza Arsenal ni kutoka kwa beki wao wa kati Koscienly

Baada ya yeye kutoka aliyeingia hakuwa na uwezo wa kuwa kiongozi imara
pale katika eneo la beki .

Ndiyo maana hata magoli ambayo yalifungwa kuanzia la pili yalikuwa
yanatokea kwenye makosa yake.

Uwepo wa Alonso na Vidal eneo la katikati lilimpa shida sana Francis
Coquelin. Jana kwa kiasi kikubwa hakuwa na mchezo mzuri.

Hakutimiza majukumu yake muhimu ya kulinda safu ya ulinzi na kuanzisha
mashambulizi kitu ambacho Xhaka kilikuwa kinampa nafasi ya yeye kuja
kumsaidia kukaba na kusahau jukumu lake la kugawa mpira kwa watu wa
mbele.

Hali iliyofanya timu ikose muda wa kuwa na mpira kwa wakati mwingi.

Bayern Munich, walinufaika sana na kuanza na viungo watatu.

Alonso alikuwa anatimiza vzur majukumu yake ya kulinda Beki yao ambayo
kwa kiasi kikubwa hawana beki ngumu.

Vidal alileta balance nzuri ya kushambulia na kukaba maana alikuwa
anaenda mbele kushambulia na kurudi nyuma kukaba. Alonso na Vidal
walimpa uhuru Alcantara kuwa katika eneo la mbele, hivo kuongeza idadi
ya watu wanne mbele kitu ambacho kilikuwa hatari kwa Arsenal hasa
baada ya Koscienly kutoka.

Kuwaanzisha Costa na Robben kuliwafanya mabeki wa pembeni wa Arsenal,
yani Gibbs na Bellerin kutokuwa na uwezo wa kupanda mbele kwenda
kusaidia mashambulizi na muda mwingi walikuwa wamekaa nyuma kujilinda
zaidi

NILICHOKIONA KWENYE MECHI YA PSG DHIDI YA BARCELONA.

Kati ya vitu ambavyo jana nilikuwa napata shida navyo kabla ya mchezo
wa PSG na Barcelona ni kutokuwepo kwa Thiago Silva pamoja na Thiago
Motta.

Lakini Marquinhos na Kimpempe jana walinifanya nimsahau kwa muda
Thiago Silva. Walicheza kwa uelewano mkubwa sana na kwa nidhamu ya
hali ya juu, kikubwa utulivu mkubwa ulikuwa ndani yao,huku Marquinhos
akiwa kiranja mzuri wa Kimpempe.

Rabiot ndiye aliyekuwa mwaandaji wa sherehe ya jana. Kwani kwa kiasi
kikubwa alifanikiwa kwanza kuilinda safu ya ulinzi ya PSG kwa kiasi
kikubwa.

Pili, ndiye mtu ambaye mashambulizi yalikuwa yanaanza kujengewa kupitia kwake.

Tatu, Uwepo wa Rabiot na Verrati kuliwanyima uhuru sana Sergio na
Iniesta, kitu kilichosababisha Iniesta kutotoa huduma ya mipira kwa
kina Neymar, Messi na Suarez hali iliyompelekea wao wao kutoonekana
kwa kiasi kikubwa katika mechi ya jana.

Nidhamu ya PSG wakati wa kushambulia na wakati wa kukaba ilikuwa ya
hali ya juu na hii ndiyo iliyowatofautisha wao na Barcelona.

Wakati PSG walipokuwa wanakaba walikuwa wanahakikisha njia za mpira
zikiwa haziko wazi, hali iliyowafanya Barcelona kukosa njia za
kupitishia mipira pindi walipokuwa wanashambulia. Ilihali Barcelona
ilipokuwa inakaba ilikuwa inaacha wazi njia za mipira hali iliyokuwa
rahisi kwa PSG kupitisha mipira na ikizingatia wachezaji wao wa mbele
walikuwa wabunifu sana.

Ubunifu wa wachezaji wa mbele wa PSG haukuweza kudhibitiwa na
wachezaji wa Barcelona kwa kuwaachia kuwa huru sana ( Yani hawakuwa
wanawakaba man to man ili kuwaghasi). Lakini hiki kitu kilikuwepo
kwenye ukabaji wa PSG, licha ya kwamba PSG walikuwa wakikaba njia za
mpira pia walihakikisha hawawapi nafasi ya wachezaji wa Barcelona kuwa
huru kwa kuwakaba man to man.

Nidhamu kubwa ya ushambuliaji waliyokuwa nayo jana PSG ni ile hali ya
wao kutumia nafasi waliyokuwa wanaipata ( kutumia hata foul walizokuwa
wanatumia hii ilikuwa inaonesha ni hali gani walikuwa na nidhamu ya
ufundi )

Pengo na Mascherano lilikuwa linaonekana kwa kiasi kikubwa jana.
Combination ya Pique na Umtiti ilikuwa haiko vizuri sana jana na ni
moja ya sababu ambayo iliwafanya Barcelona wapoteze mechi ya jana

Matokeo Mengine ya mechi ya jana

Benfica 1 vs Dortmund 0.

katika mchezo huu tulishuhudia mshambuliaji wa Dortmund raia wa Gabon,
Pierre Emir Aubameyang akikosa penalty.

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya martinkiyumbi@gmail.com

Exit mobile version