*Ghana wawabania Ujerumani kwa sare
*Argentina wasotea ushindi kwa Iran
Nigeria wamechanua kwa kuwafunga Bosnia-Hercegovina 1-0 na kuwaondoa kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Bao pekee la Nigeria lilifungwa na mshambuliaji wa Stoke ya England, Peter Odemwingie nusu ya pili ya kipindi cha kwanza.
Huu ni ushindi wa kwanza wa Nigeria kwenye Kombe la Dunia tangu 1998 na lilikuja dakika saba baada ya mshambuliaji wa Bosnia na Manchester Ciry, Edin Dzeko kukataliwa bao alilofunga kimakosa.
Nigeria watavuka hatua ya makundi iwapo watakwenda sare na Argentina au Iran watashindwa kuwafunga Bosnia.
Odemwingie amerudi kikosini miaka miwili baada ya kuwa nje kutokana na kukosana na kocha Stephen Keshi.
GHANA WAWABANA UJERUMANI 2-2
Ghana wamepigana kiume na kutoka sare na Ujerumani katika mchezo mkali.
Mechi hiyo ilishuhudia Moroslav Klose wa Ujerumani akiifikia rekodi ya mabao 15 katika historia ya michuano hiyo ya Ronaldo de Lima.
Ujerumani wamefikisha pointi nne huku Ghana wakiwa na pointi moja. Marekani wana pointi tatu wakati Ureno hawana pointi.
Ujerumani walianza kufunga kupitia kwa Mario Gotze kabla ya Andre Ayew kusawazisha na Asamoah Gyan kufunga la pili.
IRAN NUSURA WAWAAIBISHE ARGENTINA
Iran wameonesha kwamba si timu ya kudharauliwa, kwani imewachukua Argentina dakika 91 kupata bao pekee na la ushind.
Lionel Messi ndiye alifunga bao hilo baada ya jaribu jaribu za hapa na pale na kukosa, huku Iran wakisimama imara.
Iran walikwenda sare na Nigeria katika mechi ya kwanza na baadhi ya watu wakawa wanawalaumu Nigeria kwa ulegelege kumbe Iran wamebadilika.