Menu
in , ,

NI WAKATI WA TIMU ZA ENGLAND KUTAWALA UEFA?

Waweza kujiuliza ni lini ilikuwa mara yako ya mwisho kwa Ashley Young
kumuona akiwa uwanjani? Jibu utakalolipata hutokubaliana kabisa na
kiwango ambacho alikionesha katika mechi ya jana dhidi ya FC Basel
hakiendani na ukweli kwamba mchezaji huyu alikuwa nje muda mrefu
kutokana na majeraha.

Alikaba vizuri kama jukumu lake la kwanza kama beki wa kulia, pili
alikuwa anasaidia kushambulia vizuri kitu kilichosababisha yeye kutoa
pasi ya mwisho ya goli.

Unaweza ukamchukia, ukamtukana upendavyo kwa sababu hana soka la
kukufurahisha ila yeye ni mmoja wa wachezaji wanaotimiza majukumu
wanayoelekezwa na kocha na ndiyo maana Mourinho hudiriki kusema
hujiona dhaifu bila Fellain.

Ulimtazama Blind alivyokuwa anashambulia vizuri na krosi zake zenye
macho? Ulimtazama pia Young alivyokuwa anakaba na kupiga krosi zenye
macho? Hii ndiyo tofauti kubwa kati ya Young na Valencia. Valencia
mara nyingi krosi zake huwa hazina macho ukilinganisha na za Ashley
Young.

Walibezwa sana walimpoleta Bakayoyo na kumwacha Matic, walitaniwa
sana walimpomkosa Oxlaide Chamberlain na kumleta Davie Zappacosta
lakini usiku wa ulaya umedhihirisha ni kwa kiasi gani sajili zao
zilikuwa na tija.

Ujio wa Zappacosta unaweza ukawa mwiba mchungu kwa Moses. Anajua
kuweka uwiano mzuri wa kushambulia na kuzuia. Pia anapokuwa
anashambulia anakuwa na madhara makubwa sana kwa mpinzani. Usiku wa
jana kafanikiwa kufunga goli moja na kutoa pasi ya mwisho moja, kitu
hiki ni nadra sana kukiona kwa Moses.

Iliwahi kuwepo MSN, ilitisha kwa kiwango kikubwa. Ilifunga magoli ya
kila aina, Ilifunga magoli ambayo walikuwa wanayataka wao.

Mabeki wengi walikuwa wanauogopa utatu huu kila walipokutana nao.
Kila kipa alikuwa makini kila alipokuwa anajua leo anaenda kukutana na
MSN, umakini ambao haukuzia MSN isiwanyanyase makipa wengi.

Huruma kwao haikuwepo, kila muda walikuwa wanawaza kufunga goli
nyingi ipasavyo.

Marouane Fellaini, akifurahia goli lake la kufungua ‘account’ man utd..

Kila muda unaposogea unaruhusu mabadiriko mengi kutokea, ndiyo maana
leo hii hakuna MSN tena ila kuna MCN hii ni tishio jingine la mabeki.

Mbappe, Cavanni na Neymar wamejaribu kutengeneza ushirikiano mzuri
ndani ya mechi mbili tangia waanze kucheza pamoja hali ambayo
inaashiria kuwa ushirikiano huu utakuwa mwiba mwingine mchungu kwa
mabeki wa timu mbalimbali.

Kwenye karatasi inaonesha umri wa Messi unasogea sana, lakini kadri
umri wake unavyozidi kusogea ndivyo kiwango chake kinavyozidi kuwa
kitamu.

Kwa sasa Barcelona ameibeba mgongoni mwake, kila dhaifu la Barcelona
linafichwa na ubora wake.

Magoli yake mawili yalikuwa msaada mkubwa kwa timu yake Kuweza
kushinda magoli matatu kwa bila dhidi ya wanafainali wa UEFA wa msimu
uliopita yani Juventus.

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya martinkiyumbi@gmail.com

Exit mobile version