Kama kuna kibarua kinachawakabili Man United basi kumzuia Erlin Haaland asilete madhara katika lango lao
KWA mara nyingine tena katika msimu huu mashabiki watashuhudia pambano kali na kusisimua baada ya mechi za Ligi Kuu. Mechi mbili za EPL zilionesha Pep Guardiola wa Man City yungali anapigania ufalme na uwezo wa kudumisha anao, lakini Eric Ten Hag wa Man United alikuwa anatishia ufalme huo.
Wakati Man United ikifurahia kufuzu hatua ya Ligi ya Mabingwa, wenzao Man City wapo fainali ya Ligi hiyo na tayari wametwaa taji la EPL, huku wakifukuzia taji la pili kama ilivyo kwa Ten Hag. Fainali ya FA hivi leo inakuja katika kipindi ambacho Man Unied wahaha kurudisha ufalme wao wa jiji la Manchester uliochukuliwa na majirani zao City.
Ni fainali ambayo inakutanisha vita vikali ndani ya dimba; kuanzia ufundi,wachezaji, viongozi na zaidi kila mmoja anapenda kuona timu yenye uwezo wa kushindana na Man City na kuichapa kwenye fainali.
Ten Hag vs Pep Guardiola
Alipokabidhiwa jukumu la kuinoa Man United, Eric Ten Hag alisema watu wanaweza kushuhudia mwisho wa zama za ufalme wa Man City na Liverpool. Kwa mechi nne alizokutana na Man City (mbili) na Liverpool (mbili) makocha Jurgen Klopp na Pep Guardiola walimfundisha kazi ya kiufundi ambapo Man United ilipata vipigo vikali sana. Bado imani ya Eric Ten Hag iko palepale kwani Liverpool wametupwa kwenye mashindano ya Europa League kwa msimu ujao baada ya kuvurunda vibaya kwenye EPL msimu.
Kiufundi makocha hawa wameonesha ubavu mkubwa kwa mifumo tofauti. Man City wao wanacheza mpira wa drafti kana kwamba ni kazi rahisi, lakini wanabanwa na mifumo ya Guardiola hivyo vipaji vyao hubanwa. Kwa Man United licha ya mifumo bado timu yao inahitaji uhuru wa kiuchezaji ambao Ten Hag anaonekana kutoridhika na baadhi ya huduma za wachezaji wake.
Katika mfumo wa 4-3-2-1 Ten Hag amekuwa akishambulia zaidi kutokea pembeni ambako wachezaji wake watakutana na mabeki wenye roho yap aka kama Kyler Walker na Manuel Akanji au Nathan Ake. Guardiola amekuwa akitumia mfumo wa 3-4-2-1 ambao unamfanya Erlin Haaland kuwa mshambuliaji wa mwisho mwenye jukumu la kucheka na nyavu tu. Ni ufundi upi utatia for a leo?
Nani kumkaba Erling Haaland
Kama kuna kibarua kinachawakabili Man United basi kumzuia Erlin Haaland asilete madhara katika lango lao. Pengine mabeki wa Man United waliangalia mechi ya Man City dhidi ya Real Madrid zote mbili kugundua mbinu walizotumia kumdhibiti Erling Haaland ambaye hakupata nafasi ya kufunga bao.
Mabeki Antonio Rudiger, Eder Militao na David Alaba wote katika mechi mbili walimdhibiti Haaland kwa kuhakikisha hapati nafasi hata hatua mbili. Wapishi wake walibanwa kiasi kwamba walitakiwa kutoa pasi kwa wachezaji wengine.
Kwenye mchezo wa marudiano Pep Guardiola akazlimika kuongeza nguvu katika mfumo na kuwanyima wachezaji kuonesha vipaji vyao vya asili, na ndio maana Kevin De Bruyne alilazimika kumfokea kocha wake akae kimya kwa sababu alikuwa anaelekeza na kulaumu kupindukia badala ya kuruhusu kazi ifanyike hata kwa vipaji binafsi.
Kazi ya mabeki wa Man United ni ngumu, na itajulikana leo ni mbinu gani watatumia kumdhibiti Erlin Haaland ambaye mashabiki wa Tanzania wamempachika jina la ‘Jini’ kutokana na kasi yake ya kufunga mabao.
Man United wana hasira zaidi
Ni timu inayorudisha ufalme wake, lazima wahakikishe wanatwaa kombe hili na kuwapa amani mashabiki wao. Man United wana hasira nyingine kuona rekodi ya kupachika mabao ya mshambuliaji wao wa zamani Andy Cole ikivunjwa na Erling Haaland. Tena imevunjwa na mchezaji wa timu ya watani wao wa jadi. Hasira iliyoje. Dawa wanawyoweza kutumia ni kuwafunga Man City ili kuziba kelele za wao kuwa waflme wa jiji la Manchester. Je Man United watafanikiwa kibarua hiki?
Pesa ya waarabu vs wamarekani
Man City wanatamba katika soko la manunuzi ya wachezaji. Wanatembea vifua mbele. Lakini siri yao kubwa ni pesa za waarabu ambao wanamiliki timu hiyo. Matajiri wao wanasajili wachezaji wakali zaidi na kuifanya kuwa timu ya kuogopeka.
Man United wao wanahasira na utawala wa pesa za Kimarekani, ni kama vile zina gundu kwa sababu hawajafanya mambo makubwa katika mchezo wa soka tangu wamarekani hao walipoinunua timu hiyo.
Familia ya Malcolm Glazer ipo kwenye hatua za kuiuza Man United na hivyo kuondoka. Lakini fainali ya leo inakutanisha pesa za waarabu dhidi ya pesa za Wamarekani. Ni pesa zipi zitatamba baada ya dakika 90? Au labda dakika 120? Ni jambo la kusubiri na kuona.