Kitu kibaya zaidi kuhusu anguko la Manchester City ni kwamba wametaka wenyewe, inaonekana kama hawajifunzi. Man City wakati wanatupwa nje ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Olympique Lyon, si muda mrefu umepita, Kevin De Bruyne alikiri “Mwaka mwingine, mambo yaleyale,” na inaonekana hakuna mabadiliko yoyote ndani ya klabu hiyo.
Hilo lilitosha kuonesha uchambuzi wa De Bruyne kuwa kuna kasoro ndani ya klabu hiyo. Yeye ni mchezaji ambaye alipiga kelele baada ya kipigo cha jumapili iliyopita kutoka kwa mabingwa wa zamani wa EPL, Leicester City, lakini kwa maneno yake ni dhahiri yanakuwa maarufu na yanaonesha namna kiwango cha Man City kilivyo kwa kwa kipindi hiki.
Masikitiko hayo ni ushahidi kama sauti ya Barry Devies wakati akitangaza kutolewa kwa timu ya taifa ya Italia kwenye mashindano ya fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002, alisema, “…na Italia nao wametupwa nje kwa sababu walikuwa tayari kwa hilo. Wapo tu, hawajifunzi,”
Wakati gani Man City kama timu watajifunza?
Hii ilikuwa mara ya kwanza timu ya Pep Guardiola kufungwa mabao matano, lakini ni mara ya pili kwa Jamie Vardy kufunga mabao matatu dhidi ya kocha huyo maarufu duniani.
Mara ya kwanza ilikuwa msimu wa kwanza Pep Guardiola kuinoa Man City, ulikuwa usiku ambao kikosi cha Man City hakikuwa na jambo jipya wala kuwa karibu na kiwango chao. Kikosi chake hakikuwa tayari kutumikia mbinu alizoweka kusaka ushindi.
Ukiangalia kipigo alichopata wikiendi iliyopita ni aina ileile ya vipigo vingine alivyowahi kukutana navyo miaka iliyopita. Hilo linaweza kuthibitisha kuwa Man City hawaonekani kuwa imara kipindi hiki. Kilichopo ni uzoefu na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja.
Tunaweza kuangalia ubora wa kikosi na namna kocha wao anavyotoa maelekezo pembezoni mwa uwanja, na hakika inashangaza ni kwanini Man City wanapata matokeo mabovu. Tukiwatazama tuona wamewahi kuwa na misimu miwili bora katika Ligi Kuu England, fedha wanazotumia, miundombinu yao bora, mfumo wa uongozi na kivutio kizuri zaidi ni uchezaji wao, wachezaji wapya wanaosajiliwa, licha ya kujua maeneo waliyotaka kuboresha inashangaza hali ya matokeo yao kwa sasa.
Hata hivyo, Brendan Rodgers amejaribu mara kadhaa kuichapa Man City kwa kipindi cha misimu minne iliyopita, lakini ni mmoja pekee ndiyo amefanikiwa kuinyanyasa Man City licha ya utajiri wao.
“Man City wana kikosi kizuri kinachoweza kuhatarisha mabeki wako wanne. Kadiri unavyowashambulia ndivyo wanavyobadilika kimbinu, wana uwezo mkubwa wa kimbinu, wakati mwingine huwezi kuwapa presha wachezaji wao walionao. Wanauchezea mpira kila kona, wanasonga mbele, wanaziba nafasi na kutumia minya kupata ushindi. Watu hawawezi kuziona timu nyingine zikicheza kama Man City, lakini nilifikiria mchezo wetu dhidi yao ulikuwa kwenye jicho la kiufundi na kumtoa langoni golikipa wao. Ederson amecheza mechi kadhaa kama beki wa kati wa Man City, ni beki wa mwisho kikosini, ni mzuri anapokuwa na mpira, kwahiyo ilibidi tucheze kwa kuwaweka wachezaji nusu ya eneo letu badala ya robo tatu, tuwangojee waje, ili tuzibe mianya ya nafasi, kisha tunawashambulia kwa kushtukiza. Swali lilikuwa tuna nyenzo ya kutumia kupiga pasi ndefu kuvuka eneo lao la katikati na kuwavuruga? Nashukuru tulifanikiwa kufanya hivyo kwa kiwnago halisi,” alisema Brendan Rodgers.
Leicester City walifanikiwa, wakaongeza kasi ya kufanikiwa kuwachapa mabao matano. Kocha wao Brendan Rodgers pengine alifurahi zaidi kutamka maneno hayo ambayo bila shaka yatawafanya bodi ya Man City kukaa chini na kuchambua mwenendowao msimu huu. Lakini, kw aufupi, Leicester City waliifunika kabisa Man City. Walihakikisha wanatumia udhaifu wa wachezaji bora wa Man City na kuwatia presha kila upande.
Mara ngapi Man City wamehaha kuzifungua timu zinazolinda nusu ya eneo lao na kupiga pasi ndefu za juu kwenda pembeni au katikati kwa kasi na kuwafanya vijana wa Pep Guardiola wakichanganyikiwa kwa namna wanavyoshambuliwa? Matatizo hayo yaliwatokea Man City msimu uliopita wakati walipochuana na timu za Norwich City, Liverpool, Wolverhampton Wanderers, Manchester United, Tottenham Hotspur na kwenye Ligi ya Mabingwa dhidi ya Olympique Lyon.
Umahiri wa Man City ni namna wanavyopigiana pasi kuelekea lango la adui, ni tishio kubwa kwa timu mbalimbali. lakini kikosi cha Leicester City kama alivyosema Brendan Rodgers kuhakikisha wanawaondoa kwenye maeneo yao. mara walipofanikiwa hilo mchezo mzima ukawa mikononi mwa Leicester. Man City wanafahamu Rodri anahitaji muda kumudu namna ya kukabiliana na kasi ya wachezaji wanaomkimbiza, lakini hawakutegemea kuona wachezaji zaidi ya wawili wanamkabili beki hiyo wa Kihispania. Leicester City walimtumia Rodri kama nyenzo yao ya kuivuruga Man City.
Hata hivyo washambuliaji na viungo wa Man City wanatakiwa kuongeza viwango vyao ili kuleta matokeo mazuri kwao, kwa vile haitoshi kuwalaumu mabeki wao kwa matokeo mabovu wanayopata.
Lakini safu ya ulinzi kuna swali linatakiw akujibiwa; “ni namna gani hali imekuwa hivyo?’ John Stones hajafanikiwa, majeruhi Benjamin Mendy hajafanya kile kilichotarajia; kuibuka Oleksandr Zinchenko kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza, mwanzo ilionekana dalili njema, lakini amekuwa mchezaji wa ziada na huenda akaondoka msimu huu. Kwahiyo unaweza kuona kile walichokiona kwa Nicolas Otamendi miaka mitano iliyopita (mzuri kwenye mpira, nguvu za kutosha, na beki kisiki), lakini alikuwa na msimu mmoja mzuri na sasa anaelekea kuondoka klabuni hapo. Kwa Joao Concelo kuumia mara kwa mara ni tatizo kubwa, lakini alisajiliwa kwa sababu Danilo aliychukuliwa baada ya kumkosa Dani Alves mwaka 2017 alitaka kuondoka Etihad. Angelino ni mchezaji wa kuziba pengo, lakini walimpeleka kwa mkopo tena kabla ya kusajili mchezaji mwingine za kuziba nafasi yake.
Man City wamefurahia kiwango cha Kyle Walker na Aymeric Laporte, na imekuwa kazi nzuri ya Mfaransa huyo kwa sababu ya uamuzi (na ulikuwa uamuzi haswa) wa kusitisha kumnunua aliyekuwa beki mahiri wa Southampton, Virgil van Dijk kwa sababu ya bei yake kuwa kubwa zaidi. lakini hilo likawasaidia Liverpool kumsajili beki huyo ambaye amekuwa kinara wa mafanikio ya klabu hiyo.
Iko wapi Man City kwa sasa? Ni kikosi kizuri sana, lakini kuna hatari zinakuja ambazo si za kubezwa. Ni kweli kwamba Man City wameanza msimu huu wakiwakosa wachezaji saba au nane muhimu wakiwa majeruhi, wakiwemo washambuliaji wawili na hilo limetokana na mechi za maandalizi ya msimu. Man City waliwafunga Wolves jumatatu kwa mabao 4-0, lakini kichapo kutoka Leicester kinapaswa kuangaliwa kwa muktadha mwingine.
Wakati huo, matatizo hayo yakiwamo, na klabu inatakiwa kuboresha baadhi ya mambo msimu huu kwa sababu mara baada ya kumaliza msimu uliopita walitaka kusajili mabeki wawili wa kati,winga mmoja, mshambuliaji mmoja na winga wa kushoto.
Inasemakana kwamba Eric Garcia, mwenye umri wa miaka 19 ambaye anataka kuondoka klabuni hapo, naye anatakiwa kupewa nafasi kikosi cha kwanza.
Pengine kwa kiasi fulani wanaweza kulalamikia majeruhi walinao. Laporte hajaimarika tangu alipotoka karantini ya corona, lakini John Stones anasumbuliwa na misuli hata hivyo si jambo la kuwaathiri Man City kwa vile hawatarajii kumtumia kikosini msimu huu.
Labda, Mn City wameshindwa kuanz amaisha bila John Stones, na wanaweza kuwa na sababu kwanini hawakulipa kiasi cha fedha kilichotakiwa na Napoli ili wamsajili beki wa kati Kalidou Koulibaly, na kwanini Otamendi ajumuishwe kwenye mpango huo wa usajili. Kama Sevilla waliomhitaji Otamendi wangemsajili, ingewawezesha City kumsajili Jules Kounde, lakini hawakufanya hivyo. Kwahiyo raia huyo wa Argentina, Jules Kounde anaelekea kuwaimarisha Benfica, ambao kutokana na matatizo ya kifedha ina maana wasingeweza kukataa dau la kununuliwa Ruben Dias, mchezaji waliyemfuatilia kwa miezi 18 iliyopita, lakini hakuwa mchezaji mwenye kupewa kipaumbele cha kusajiliwa klabuni hapo.
Mashabiki wanaumia kusikia klabu yao bado inatafuta beki wa kushoto, lakini haina maana kuwa ni muhimu kumsajili yeyote kwa vile nafasi hiyo itakuwa ya Zinchenko miaka ijayo.
Nyota huyo kutoka Ukraine amekuwa akitakiwa na klabu mbalimbali, ikiwa moja itakubali kulipa dau wanalotaka Man City, ina maana Guardiola atakuwa na nafasi ya kuboresha eneo hilo.
Jambo lingine la kuchungwa zaidi ni mabeki wao watatu kusababisha penati. Viungo wao wanaruhusu kushindwa kwa urahisi, wachezaji wa City wanashindwa kukimbia kilometa nyingi wakati wa mchezo.
Kyle Walker alisababisha bao la kwanza. Garcia, alikuwa mchezaji mzuri kipindi cha kwanza, akawa mbaya zaidi kipindi cha pili, na akasababisha bao la pili.
Mendy aalijipanga vibaya na kumfanya madhambi James Maddison hivyo kuwa penati ya tatu iliyohitimisha mabao 5-2. Iko hivi, wakati matokeo yakiwa 3-1 huku zikisalia dakika 30 kimalizika mchezo, hakukuwa na dalili zozote kwa Man City kusawazisha mabao hayo. Jitihada zao zilikuja pale walipofanikiwa kupata bao la pili, huku wakiwa wamezabwa 4-2, kabla Mendy kuwapa bao la tano Leicester City.
Hii ni mara ya kwanza kwao kuruhusu timu iwafunge mabao matano. Hii ni mechi iliyoonesha Gaurdiola akikata tamaa, na huenda hakutarajia kipigo kikubwa namna hiyo. Bila shaka anashangaa nini kinachoendelea katika kikosi chake, na kwanini wachezaji wenye vipaji vikubwa namna hiyo wanaruhusu mabao matano.
Hata hivyo Guardiola mwenyewe aliwashangaza wengi kwa kumtoa Fernandinho, mchezaji anayelinda mabeki wake na kumwinginza kinda mwenye umri wa miaka 17 Liam Delap. Wakati Delap anaingia katika dakika 51 matokeo yalikuwa 1-1. Makosa hutokea kwa makocha na hili ni miongoni mwa makosa ya Guardiola, ambaye ana kikosi chenye wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu.