Menu
in

Newcastle United ni habari ya mjini sasa

Tanzania Sports

Tajiri mpya kaingia mjini. Hiyo ndiyo kauli inayofaa kutumika katika dili la ununuzi wa klabu ya Newcastle United. Umiliki wa miaka 14 wa tajiri Mike Ashley umefika tamati, baada ya Newcatsle United kutangazwa kununuliwa na tajiri kutoka Saudi Arabi.

Nani mmiliki mpya?

Ni Saudi Arabia kupitia Saudi Public Investment Fund. Dau la kumiliki Newcastle United ni pauni milioni 300 zimetumika kukamilisha dili hilo. Ifahamike ununuzi huo ni mkubwa zaidi mara 11 ya ule uliofanywa na Sheikh Mansour wakati anainunua Manchester City.

Ifahamike mwaka mmoja uliopita wamiliki hao walishindwa kuinunua Newcastle kutokana na mgogoro wa kisheria za haki za kuonesha Ligi Kuu England nchini Saudi Arabia. 

Televisheni ya beIN Sports ambayo inamiliki haki za televisheni za ligi ya England nchini Saudi Arabia ililalamika kulikuwa na chaneli ya mtandaoni ambayo ilionesha mechi za Ligi Kuu England kwa njia haramu (bila idhini) yao. 

Kwa beIN Sports waliamini kuwa chaneli hiyo ilikuwa chini ya ufadhili wa serikali kwa miaka mingi kuonesha mechi bila idhini. Hicho kilikuwa kikwazo ambacho kilichangia ununuzi wake kuwa mgumu. 

Masharti ya England kwa wamiliki wapya yalikuwa ni kuthibitisha kuwa hawana uhusiano na chaneli iliyokuwa inaonesha EPL bila idhini. 

Nani atakuwa bosi mpya?

Mabadiliko ya umiliki wa timu au taasisi au kampuni yoyote lazima uongozi mpya uingie. Kwahiyo Newcastle United nayo inatarajiwa kumpata bosi mpya Yasir Al-Rumayyan ambaye atakuwa rais mtendaji wa timu hiyo, ambaye ameshangiliwa na mashabiki wa timu hiyo mitaani baada ya kumaliza utawala wa Mike Ashley.

Aidha, katika muundo wa uongozi inatarajiwa wengi watakuwa wanatoka England hapo hapo, kwa sababu Saudi Arsbis imethibitisha kisheria kuwa hawakuwa katika safu za uongozi wa ndani wa klabu hiyo.

Noti za usajili kumwagwa

Bila shaka tajiri mpya atasajili wachezaji wapya,makocha wapya,viongozi wapya,mwelekeo mpya nap engine ndiyo mwanzo wa historia mpya ya klabu hiyo kongwe nchini England. 

Ndiyo, Newcastle United ni klabu kongwe na yenye sifa nyingi katika soka England kabla ya kudorora miaka ya karibuni. Hii ndio klabu iliyowahi kummiliki supastaa Alain Shearer ambaye alikuwa moto wa kuotea mbali. 

Hata hivyo hoja yangu si ustaa wa Shearer bali namna Newcastle United inavyogeuka kuwa Man City mpya au PSG mpya katika ulimwengu wa kandanda. 

Mwelekeo mpya

Tajiri anavyoingiza pesa za uwekezaji maana yake kuna mambo mapya yatakuwepo nap engine yale ya mmiliki wa zamani yatafutiliwa mbali. Swali linalobaki ni upi mwelekeo wa Newcastle kwa sasa baada ya akaunti zao kunona pesa?

Ni wazi kipindi cha usajili kijacho cha mwezi januari kutakuwa na pilika pilika nyingi ndani ya klabu hii. Vurugu za usajili zitakuwa na maana nafasi ya kocha wa sasa itakuwa shakani, wachezaji wa sasa watakuwa shakani, na itakuwa ni dhahiri kuwa timu itahitaji mwelekeo mpya kuliko hali ya sasa.

Newcastle United wanashika nafasi ya tatu za mwisho za msimamo wa Ligi  baada ya kupata pointi tatu pekee kati ya mechi 7 walizocheza msimu huu. Hilo ni jambo la hatari ikiwa na maana uongozi mpya utakuwa na lengo la kutengeneza mwelekeo mpya katika taswira yao ya soka.

Yupi kuwa nyota wa kwanza kutua?

Wakati Manchester City ikitangazwa kununuliwa na matajiri wa kiarabu, swali hilo liliibuka na nyota kadhaa walisajiliwa. Miongoni mwao ni Robinho ambaye alitoka Real Madrid, kisha wakafuata wengine akina Emmanuel Adebayor, Raheem Sterling na wengineo. 

Hata nafasi ya kocha nayo akatafutwa mwingine. Nafasi ya watendaji wakuu ilichukuliwa na wengine hivyo waliokuwepo enzi za Thomas Cook waling’olewa na wamiliki wapya. 

Kwa maana hiyo Newcastle United inaingia katika njia ileile ya PSG na Manchester City ambapo pesa hazikutawa tatizo, badala yake nafasi za ajira huenda zikapata watendaji wapya hasa zile za kuingia uamuzi na mustakabali wa timu hiyo. 

Sasa nyota hyupi atakuwa kwanza kusajiliwa Newcastle? Hilo ndilo swali linaloulizwa zaidi kwa sasa. Je atakuwa Kylian Mbappe.Erlin Halland,Lionel Messi,Neymar? Karim Benzema? Lewandowski? Manuel Neuer? Muda nao utaongea.

Kocha mpya Newcastle atakuwa nani?

Vyovyote vile iwavyo Newcastle Unitrd itaingia sokoni kuajiri kocha mpya kulingana mazingira ya mmiliki mpya. Kwa haraka makocha Antonio Conte, Ronald De Boer,Zinedine Zidane, Andre Pirlo hawana timu kwa sasa, hivyo karata inaweza kuwaangukia wao. 

Hata hivyo huenda ikawa rahisi kuwapata Conte na Pirlo kuliko Zidane mwenye utamaduni tofauti wa kazi yake. inafahamika ndoto yake iliyobaki ni kuifundisha timu ya taifa ya Ufaransa. Hivyo kumshawishi kuwa kocha wa Newcastle ni jambo linalohitaji nguvu za kutosha. Kwenye soka lolote linawezekana.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version