*LIGI Kuu England imeanza kama kawaida huku timu zikiwa kwenye harakati za kuibuka na ushindi. Kila timu inajaribu kujenga kikosi chake lakini vita kubwa itakuwa ni kuingia kwenye Top Four.
MANCHESTER CITY
Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo wakiwa nanakwenda kwa mwendo wa taratibu zaidi. Bila shaka wanatarajiwa kufanya vizuri kutokana na kikosi chao kukaa pamoja zaidi. Stefan Jovetic ataibuka kuwa mshambuliaji muhimu kutokana na jinsi anavyoonesha kwa sasa.
Man City wamekuwa na kikosi kilekile wanachokiamini na kuingi kwa Fernando kutaongeza nguvu ingawa si kiasi kikubwa lakini kazi itakuwa kupigania to four.
MANCHESTER UNITED
Jana Louis van Gaal amekuwa na mechi ya pili iliyoisha kwa sare ya moja kwa moja. Kikosi cha Man United bado kinaonekana hakijaamka na kucheza soka kwa kiwango cha kuridhisha.
Usajili wa Marcso Rojo ni mzuri na unaweza kuisaidia zaidi timu hiyo sambamba na Luke Shaw. Rojo ana kipaji, ni beki hodari na mwenye kushambulia kwa akili.
Tatizo kubwa la kikosi hicho ni mfumo wa 3-5-2 anaotaka kocha wa Manchester United anahitaji wachezaji wenye ubora zaidi angalau watano.
ARSENAL
Kuingia kwa nyota kadhaa kutaimarisha kikosi hicho Alexis Sanchez, Calumn Chambers na Martin Debuchy wameingia kikosi cha kwanza, lakini Arsenal wana kiungo mkabaji mmoja tu, Mathieu Flamini.
Joel Campbell ni namba kumi halisi kama Lukas Podolski, hivyo kuwapanga kushoto ni sababu ya àina yao ya soka tu.
Ingawa mashabiki wanaamini kuwa kiungo mkabaji wa Arsenal atakuwa Calumn Chambers, na kwamba sasa hivi anacheza nafasi ya beki kwakuwa Per Matersacker hayuko fiti.
Ukiondoa Calumn Chambers chaguo jingine ni Abou Diaby. Kwa hakika Arsenal hadi sasa eneo hili halijapata mchezaji sahihi tangu kuondoka kwa Patrick Vieira.
Ukiangalia wachezaji waliopo Mathieu Flamini pekee anamudu nafasi hiyo. Beki wa kati nayo bado haijaimarika jambo ambalo linaleta tatizo.
Wamecheza mechi ya kwanza na kushinda, lakini Arsenal haiwezi kutwaa ubingwa kwa kuacha kuimarisha eneo la kiungo wa ulinzi.
LIVERPOOL
Ni dhahari sasa Steven Gerrard anaweza kuwekwa nje ya kikosi cha kwanza kupisha damu changa katika kikosi cha Liverpool.
Kuna nyota kama Alberto Moreno, Dejan Lovren, Lazar Markovic, Adam Lallana ni wachezaji wapya wenye kuongeza chachu ya mafanikio kikosini.
Ingawa kocha Brendan Rodgers anataka kukamilisha usajili wa Mario Balotelli bado anahitaji mshambuliaji mkali zaidi kwa falsafa yake.
Eneo la kiungo kuna Joe Allen, Lucas Leiva na Jordan Henderson wanaweza kuwa wachezaji wazuri, lakini anahitaji kiungo mwingine na beki wa kati wa uhakika.
Safu ya ushambuliaji licha ya kutegemea falsafa ya kocha huyo bado inahitaji ‘jitu’ lenye usongo wa kufumani nyavu. Anfield hawana mtu huyo tangu kuondoka Luis Suarez.
CHELSEA
Jose Mourinho hajaanza kuwa na maneno maneno kama ilivyozeoleka lakini anajenga kikosi chake kupitia kwa Diego Costa ambaye amezungukwa na viungo Fabregas, Oscar na Hazard wenye jukumu la kumtengenezea mabao.
Ukiangalia timu zote, tunaweza kusema ni mapema mno nani atatwaa ubingwa lakini Chelsea wanaweza kuwa timu tishio zaidi msimu huu.