Ikiwa imesalia miezi michache kumalizika kwa ligi kuu bara nchi imekumbwa na msiba mzito wa kufiwa na aliyekuwa raisi wa nchi Mheshimiwa dokta John Pombe Magufuli. Katika msimamo wa ligi kuu bara tano bora imepata mgeni kwani timu ya wababe wa mkoa wa Mara timu ya Biashara United iko katika nafasi ya 4 ya msimamo wa ligi hiyo. Baada ya kufikia mafanikio hayo walijikuta wamepata changamoto kwani kocha wao mkuu Francis Baraza akaanza kutamanisha vilabu kadhaa na jatimaye kujikuta anachukuliwa na timu ya inayoshiriki ligi kuu Tanzania ya Kagera Sugar kwa ajili ya kwenda kufundisha.
Kuanzia wiki ya pili ya mwezi mechi timu ya Biashara United ikautangazia umma kwamba kocha wao hawako naye tena na kwamba kocha huyo amehamia timu ya kagera sugar. Na baada ya kocha huyo kuhama timu uongozi wa timu hiyo ulitangaza wazi kwamba nafasi iko wazi na wanahitaji kocha mpya. Na waliandaa tangazo la kazi ambalo lilisambaa katika mitandao ya kijamii. Tangazo hilo liligusa hisia za wapenzi wa soka nchini ambao hawakusita kutoa maoni yao katika makundi sogozi ambayo imefanya vizuri kutangaza wazi kwamba inataka kuajiri kocha mpya kwa kutumia taratibu za kutoa tangazo la wazi na huku wakitanabaisha vigezo ambavyo wanavyovihitji huyo kocha awe navyo. Kwangu mimi naona ni mwanzo mzuri na natumai kamati yao ya ufundi itachagua kocha ambaye atakuwa na vigezo ambavyo vinaweza kuifanya timu hiyo kufika mbali. Kuna mambo kadhaa ambayo naweza kushauri klabu hiyo kuyarekebisha ama kuyaweka sawa. Mambo hayo ni kama yafuatayo:
Wafungue mtandao(website). Nilipojaribu kuingia katika mitandao kila nilipojaribu kuitafuta klabu hiyo sikuona sehemu yenye kuonyesha mtandao wa habari wa kilabu hichi. Katika ulimwengu wa sasa mandao wa kutoa habari ni kitu muhimu sana kwani mashabiki na wadau wenguine wanatakiwa wapate sehemu ambayo itakayotambulika kama ndio nukta ya marejeo pindi wanapotaka taarifa mbalimbali kuhusu maendeleo ya klabu hiyo. Kwenye mitandao ya kijamii wamejitahidi kuwa na kurasa ila baadhi ya kurasa hizo zimelala sana ukilinganisha na kurasa za vilabu vingine. Kwenye mtandao wa facebook wana wafuasi elfu tano na mia tatu na mara ya mwisho kupost ilikuwa ni januari 15 mwaka 2019
Waandae chapisho la historia ya klabu yao. Bidhaa yoyote yenye kugusa walaji inatakiwa ibebe hadithi nzuri yenye uwezo wa kuvutia watu kuifuatilia. Uongozi wa kilabu unatakiwa ukusanye na kisha kuandaa hadithi ambayo itauzika kwa mashabiki na wadau wengine wa klabu juu ye historia ya klabu hiyo. Nlipojaribu hata kuangalia mtandaoni sijaona mahala popote pale ambapo kumeelezea historia ya klabu hiyo. Nimeangalia jina lao la utambulisho la “ wanajeshi wa mipakani” sina neon juu ya neon hilo wanatakiwa waangalie namna ya mashabki na wadau wa soka kuelewa mantiki na falsafa ya msemo huo na watumie mbinu za kuweza kufanya msemo huo ukubalike.
Hayo ni mawazo yangu na nina imani wana uwezo wa kufikia hayo mawazo yangu lakini ili wayafikie hayo basi hawana budi wakae chini kisha watafute watu wa masoko na wapanue idara hiyo. Kitengo/idara hiyo kipate watu wenye uweledi ambao wanaweza kuifanya klabu iwe ni bidhaa na iweze kuuzika kwa mashabiki na wadau wengine wa klabu.
Waandae mechi za kirafiki na timu za nje wakati msimu unapoisha. Kwa kuwa sasa wao ni timu namba 4 basi wanatakiwa wajiandae kimawasiliano na timu ambazo zipo nje ya mipaka ya timu yetu kwa ajili ya kuzialika kushiriki mechi za kirafiki katika nyakati ambapo ligi itakapokuwa iko likizo. Kama wakifanikiwa kupata timu yenye jina kubwa basi watakuwa wamejiongezea wigo wa mashabiki kwani watakuwa wameongeza jina lazo zaidi.
Mwisho niwatakie mafanikio mema klabu hii na iongeze nguvu katika benchi la ufundi na wala isibweteke katika nafasi ya ligi ambayo wameifikia bali waongeze jitihada ili waweze kufika mbali zaidi.