Menu
in , , ,

Naitazama Mechi ya Chelsea na United……

 

Ni mtihani xxl, kwa David Moyes…

 

Manchester united watasafiri jumapili hii kwenda katika jiji la London kuwavaa watoto wa Jose Mourinho, Chelsea the blues. Man United msimu huu wamemfunga Arsenal tu pale Old Trafford na wameshindwa kutamba mbele ya timu zote zilizo katika nafasi sita za juu kwenye msimamo wa EPL.

Man United walifungwa na Liverpool pale Anfield, Wakafungwa na Mn city kule Etihad, huku wakipokea kichapo toka kwa Everton na Spurs nyumbani kwao Old Trafford na kulazimisha suluhu na Chelsea mzunguko wa kwanza.

Man United watawakosa washambuliaji wake mahiri, Wayne Rooney ambaye katika mechi 17 alizocheza msimu huu, ameweza kuifungia United goli 9 na kutengeneza magoli mengine 9 na pia, watamkosa Roben Van Persie ambaye amecheza mechi 11 msimu huu na kufunga magoli 7 huku akitengeneza mengine mawili. Luiz Nani, Phil Jones, Rio ferdinand na Fellain wote wataukosa mchezo huo.

Chelsea wamekuwa kwenye kiwango kizuri kwa sasa huku wakicheza mechi zao 3 za hivi karibuni bila kuruhusu wavu wao kuguswa na kumfanya golikipa Peter Cech kuingia kwenye rekodi ya kuwa kipa aliyecheza mechi 313 huku akiruhusu kufungwa magoli 234 na kumaliza mechi 150 bila kuruhusu wavu wake kuguswa. John Terry na Cahill wanaonekana kuimarika katika safu ya ulinzi.

Baadhi ya wachezaji wa chelsea FC
Baadhi ya wachezaji wa chelsea FC

Eden Hazard anaonekana kuwa moto wa kuotea mbali huku akiwa ameifungia Chelsea magoli 9 na kutengeneza mengine 5 kwenye mechi 21 alizocheza msimu huu huku Oscar Dos Santos naye akiwa ameifungia chelsea magoli 6 na kutengeneza mengine 2 katika mechi 19 alizocheza msimu huu.

Man United wanahitaji nidhamu katika mchezo huu ambao hawapewi nafasi ya kushinda, Shinji Kagawa anatakiwa kucheza kwenye ubora wake ili kuweza kumtengenezea nafasi Danny Welback ambaye kwa sasa ndiyo anayeibeba United huku akiwa ameshaifungia magoli 8 na kutengeneza moja katika mechi 15 alizoichezea united.

Carrick na Fletcher wanatakiwa kuanza mechi hiyo ambayo Mourinho anaweza kuwaanzisha Ramires na David Luiz sehemu ya kiungo kutokana na Frank Lampard kuukosa mchezo huo.

Hii ndiyo nafasi ya pekee ya David Moyes kuweza kuandika historia nzuri baada ya kuvunja rekodi nyingi ambazo Sir Alex Ferguson alikuwa ameziweka za kutofungwa pale Old Trafford.

Mourinho tangu mwaka 2004 alipotua Chelsea na kutimka mwaka 2007 kabla ya kurudi tena msimu huu, hajawahi kupoteza mchezo wa ligi kuu anapocheza nyumbani Stanford Bridge na David Moyes anauwezo wa kuvunja rekodi hiyo, japo wengi hawampi nafasi kubwa ya kufanya hivyo, kufuatia kufanya vibaya katika michezo ya United ya hivi karibuni.

51.577986-0.130329

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version