Menu
in , ,

Mwanasoka afungiwa mechi 70

*Ni Ismail Gunduz aliyempiga kichwa mwamuzi

Rekodi za utovu wa nidhamu katika soka zinazidi kuwa nyingi na chafu, ambapo mwanasoka wa Austria, Ismail Gunduz amempiga kichwa mwamuzi na kufungiwa kucheza mechi 70.

Gunduz ni mchezaji wa ridhaa aliyekuwa akikipiga katika timu ya SK Rum, na kosa lake ni kutoa mrejesho hasi dhidi ya mwamuzi baada ya kuoneshwa kadi ya pili ya njano na hatimaye nyekundu.

Hiyo ilitokea katika dakika ya 87 ya mchezo dhidi ya SPG Innsbruck West, ambapo aliishia kumpiga kichwa mwamuzi, na sasa pamoja na adhabu hiyo, Gunduz amefukuzwa klabuni moja kwa moja.

Kocha wa timu hiyo, Michael Messner ameliambia gazeti moja la Austria kwamba wanamkana mchezaji huyo kwa tabia yake chafu na tayari ametupwa nje ya timu  na klabu moja kwa moja. Adhabu hiyo imetolewa na Chama cha Soka cha Tirol kinachosimamia Tirol Liga, yaani ligi daraja la nne nchini humo. Klabu yake pia imeadhibiwa kwa kutozwa faini ya euros 257, sawa na pauni 204 au Sh 546,433.

Ismail Gunduz
Ismail Gunduz

Wachezaji wengine waliopata kupewa adhabu kubwa kwa tabia chafu na kupiga watu mchezoni ni pamoja na yule wa mpira wa kikapu, Ron Artest aliyefungiwa mechi 86, kwa kitendo chake cha kwenda kupigana na washabiki baada ya kurushiwa kinywaji uwanjani.

Chris Simon anayeshiriki mchezo wa ice hockey alifungiwa mechi 30 kwa kosa la kumpiga mpinzani wake mguuni na kifaa cha mchezo huo.

Lakini kwenye soka kuna Tran Dinh Dong aliyefungiwa mechi 28 kwa kosa la kumkabili mpinzani wake kwa nguvu na kwa makusudi kiasi cha kumvunja mguu wake.

Wengi wanakumbuka dhabu dhidi ya Luis Suarez aliyefungiwa kucheza mechi tisa za kimataifa na kuzuiwa kucheza kwa miezi mine kwa kumng’ata Giorgio Chiellini wa Italia wakati Uruguay walipocheza nao kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil hivi karibuni.

Msemaji wa Chama cha Soka Tirol, Horst Scherl amesema adhabu hiyo ni kubwa lakini inamfaa kutokana na kosa lake na kwamba angeweza kufungiwa hadi mechi 78 kwani sheria inaruhusu.

Gunduz mwenyewe amekana kumpiga kichwa mwamuzi, akidai kwamba aliteleza tu na wao kugongana vichwa, akasema adhabu hiyo ni utani na kwamba atafanya kila awezalo kurejea uwanjani mapema iwezekanavyo.
 

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version