Menu
in , , , ,

Mtanzania bingwa kuruka kamba


*Simba wakataa ofa ya Mwinyi Kazimoto
*Yanga tayari kuanika wachezaji wapya

Mtanzania aliyekulia katika mazingira magumu, Hamisi Kondo ametawazwa bingwa wa mchezo wa kuruka kamba duniani.
Kondo ambaye ni yatima, amewasili nchini Tanzania kutoka Marekani alikoshiriki mchezo huo, na kupongezwa na watu wa kada mbalimbali, wakamsifu kwa kuipeperusha vyema bendera ya taifa.
Kifuta machozi hicho kimekuja siku chache tu baada ya timu ya soka Tanzania kutolewa katika safari ya kucheza Kombe la Dunia 2014 na pia Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani, mashindano yatakayofanyika nchini Afrika Kusini.
Mchezo wa kuruka kamba hauchukuliwi kwa ushindani mkubwa nchini Tazania.
Wamarekani walifika nchini na kuvutiwa na uchezaji wa Kondo, wakampa mafunzo zaidi kabla ya kumpeleka Marekani na kuwa wafadhili wake pia.
Naibu Mkurugenzi katika Wizara ya Habari, Vijana na Michezo, Juliana Yasoda anasema mchezo huo wa kuruka kamba unakwenda kwa kasi na Wamarekani wameuvalia njuga, ambapo wanaofanya vyema wataingia kwenye mashindano makubwa zaidi.
Yasoda aliwataka Watanzania kuchangamkia michezo mbalimbali kama huo wa kamba, badala ya kukumbatia ile ya mazoea, ambayo kwa bahati mbaya hawafanyi vizuri kimataifa.
Mataifa 14 yalishiriki kwenye mashindano hayo, na zaidi ya wachezaji 100, hivyo sasa Tanzania inapeperusha vyema bendera yake katika mchezo huo.

Simba yakataa ofa ya Kazimoto

Klabu ya Simba imekataa ofa ya klabu ya Elmack ya Qatar kwa mchezaji Mwinyi Kazimoto.
Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga amenukuliwa na TBC akisema wamepigiwa simu na wakala aliyetoa ofa, akakataa kuitaja kwa madai ni aibu.
Kamwaga alisema kwamba klabu hiyo ya Qatar inamtaka, lakini hawawezi kufikiria ofa hiyo hata kidogo, kwani haifikii hata kiasi ambacho Simba husajili wachezaji wake wa kawaida
Kamwaga alisema ofa hiyo ni kama matusi kwao, na inaonesha jinsi jamaa hao wasivyo waungwana. Zaidi ya kutoridhia ofa hiyo, Kamwaga alisema mchezaji Kazimoto anatakiwa kurudi nchini kujibu mashitaka anayokabiliwa nayo ya kutoroka.
Simba ilimsajili Kazimoto kwa Sh milioni 30 ambazo hazijafikiwa hata na klabu hiyo ya Qatar. Kazimoto alioroka katika kambi ya timu ya Taifa Stars, iliyokuwa na kazi ya kufuzu michuano ya CHAN, na matokeo yake ikatolewa na Uganda kwa kufungwa mechi zote mbili nyumbani na ugenini.

Yanga kutambulisha wachezaji

Mabingwa wa soka wa Tanzania, Yanga wamesema wapo tayari kutambulisha wachezaji wapya waliowasajili kwa msimu ujao.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto amesema kwamba klabu yake itatambulisha wachezaji wapya katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro Jumapili hii.
Kizuguto anasema mechi hiyo ni muhimu kwa benchi la ufundi kuona wachezaji wameiva kiasi gani, na kocha Ernie Brandts Deogratius Munisi, Rajab Zahir, Hamis Thabit, Shaban Kondo, Hussein Javu, Mrisho Ngasa na Lenian Lusajo.
Yanga pia wanajiandaa kwa mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa, kabla ya pazia la Ligi Kuu kufunguliwa baadaye mwezi huu.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version