Kuna kila dalili ya Mwenyekiti wa Yanga Mshindo Msolla amekitingisha kiberiti dhidi ya Wanachama wa timu hiyo na GSM ambayo inaisaidia timu kusajili wachezaji nyota.
Hii yote ilitokana na maelezo aliyoyatoa juu ya usajili wa nyota wawili wa kigeni na baadae mchana akatoa ufafanuzi wake ambao bado haujaeleweka.
Kauli ya Msolla aliyoitoa hivi karibuni inawavuruga wanachama wa timu hiyo, alisema kuwa anawaomba wanachama wa timu hiyo wachangie fedha kwa ajiri ya wachezaji wawili wa kimataifa ambao wako tayari kuitumikia Yanga.
“Wachezaji wawili kigeni wapo tayari kuitumikia Yanga, kilichobaki sisi tuwape kiasi chao wanachohitaji waje, kama msimu uliopita tulisajili wachezaji kumi sasa wawili mtashindwa”alisema.
“Tuna wachezaji wa kimataifa wawili ambao tayari tumeshazungumza nao kila kitu, ila tunaomba gharama za usajili zifanywe na mashabiki na wadau ambao wamekuwa nasi kila wakati.
“Uwezo ninajua upo kwa sababu msimu uliopita walisajili wachezaji 10 mashabiki wenyewe ila msimu huu tunaomba waweze kusajili wachezaji wawili tu na utaratibu utatolewa hivi karibuni,” amesema.
Kauli hii wadau wameichukulia kama mkanganyiko kwa hesabu za Eng. Hersi Said ameshafunga rada ya usajili baada ya kuwasaini wachezaji kadhaa wakali.
Hebu tuangalie wachezaji waliowasajili GSM, usajili ghali zaidi kwa wachezaji wa ndani wa Tanzania Bakari Nondo Mwamnyeto dau lake ni milioni 230, Sarpong, Yacouba Sogne, Tuisila Kisinda, Tonombe Mukoko, Abdallah Shaibu, Carinhos, Mustapha Yassin, Zawadi Mauya, Farid Mussa, Kibwana Shomary na Waziri Junior.
Huku kocha mkuu Cedric Kaze akitarajiwa kutua nchini muda wowote huyu ni raia wa Burundi.
Katika kampeni ya uchaguzi wakati anaom,ba kura kwa wanachama ili aingine madarakani amesema kuwa ataifanya Yanga iwe inajitegemea na ikitaka jambo lake watalifanya haraka. Hadi sasa tayari miaka mitatu sasa imepita tangu aingie madarakani.
Mara kwa mara uchangiaji wa wanachama kwa timu zao unaingia katika ununuaji wa jezi, ada ya mwaka, kuingia uwanjani kushuhudia mitanange ya timu hapo ndio chanzo cha fedha kwa wanachama kwa timu yao.
Labda tuyafuate mawazo yake moja kwa moja alisema vile kwakuwa anaona kila jambo la usajili linafanywa na GSM yeye kama Mwenyekiti anahisi kuona upweke wa kuisaidia timu.
Leo ameifafanua kauli hiyo na bado ameshikilia msimamo wake juu ya wanachama kuchangia kusajili wachezaji, hii inatoa taswira mbaya kwa GSM ambao walijitanabaisha kuwa wanasajili mchezaji yoyote kutoka Afrika.
Japo nao GSM waliulizwa wakajibu kisayansi ila bado kauli ile haina afya baina yao.
Hapa kuna kitu kabisa kinaendelea ndani yake hakiko sawa kabisa.
Lakini kwa kawaida inakuwa ngumu kuamini kauli yake ina afya kiasi gani kwa wanachama wa timu hiyo huku wengine wakisubiri kuona uhalisia wa kauli yake.
Hebu tuvuke ng’ambo na fikra zetu endapo wanachama watachanga na kuwanunua wachezaji na kuchangia mishahara.
Najiuliza kama wakitoa fedha na kusajili mshahara atalipa nani ? Hakuona hapa nini kinaenda kutokea kama mshahara ukichelewa kutoka huku baadhi ya wengine wakipata kwa wakati.
Hiki kipindi cha miaka miwili Yanga wametumia fedha nyingi kufanya usajili na GSM ndio waliotumika sana kusajili ili timu hiyo ikae sawa.
Najiuliza Mwenyekiti Msolla na GSM hawawasiliani ili kauli ziwe zimaendana? hiki kipindi kigumu sana kwa Yanga hasa kuweza kurudisha imani ya kushindana na timu nyingine 17 katika michuano ya ligi kuu Tanzania Bara.
Yanga wanaelekea katika wiki ya mwananchi wanatakiwa watulie wawe kitu kimoja kauli nyingine zinazo weka nyufa katika mioyo ya wanachama sio nzuri zinaweza kuharibu furaha nzima ya wanacha ma wa timu hiyo.
Yanga inaanza ligi September 6 dhidi ya Tanzania Prison katika uwanja wa Mkapa na itakuwa mechi ya kwanza ya kimashindano, ni kweli watarudisha amani kwa Wananchi.