Menu
in , , ,

Mrundi Beraniho roho kwatu

Raia wa Burundi, Saido Beraniho anayekipiga West Bromwich Albion amesema hana bifu na wachezaji wenzake waliomzonga na hata kufikia kupigwa baada ya kusababisha kufungwa bao la kusawazisha na Cardiff hivi karibuni.

Beraniho (20) ambaye emepewa pia uraia wa England amesema kwamba hana nia ya kufungua mashitaka dhidi ya mchezaji mwenzake, James Morison aliyempiga na kwamba wawili hao walikutana, kuzungumza kidugu na kumaliza mambo.

Kocha Pepe Mel amesema anaamini kwamba kinda huyo atakuwa na msaada mkubwa katika mikakati ya klabu hiyo kuinusuru timu kushuka daraja msimu huu. West Brom walikuwa wakiongoza hadi dakika za majeruhi ambapo Beraniho alipokonywa mpira na kuzaa bao la Cardiff Jumamosi iliyopita.

Baada ya mechi hiyo lilizuka zogo kubwa hadi kwenye chumba cha kubadilishia nguo ambapo wachezaji kadhaa walimvaa Beraniho kwa madai kwamba alicheza kizembe. Hata hivyo, Beraniho ndiye aliifungia timu bao muhimu la ushindi dhidi ya Manchester United na pia bao muhimu dhidi ya Arsenal.

Beraniho alikuwa na uamuzi wa kufuatilia suala hilo kisheria ili apate haki yake na Morrison aadhibiwe kwa ngumi aliyomtwanga.
“Beraniho atakuwa muhimu sana kwetu katika mechi saba zinazokuja,” akasema Mel na kuongeza kwamba hakuna hatua zozote za kinidhamu zilzochukuliwa kuhusiana na tukio hilo.

Msemaji wa klabu alisema kutokea zogo kama hilo ni kawaida baada ya mechi kwa klabu nyingi, na kwamba hiyo inaonesha kwamba wachezaji wanajali na wasingependa kuona wanapoteza mechi.

“Wachezaji walimalizana wenyewe kama walivyolianzisha na sasa mambo yanaendelea vyema na kwa Beraniho na Morrison ni kana kwamba ni ndugu wa familia moja. Nimezungumza na Beraniho na anaonesha kujali kuliko watu wengine wa umri wake mdogo. Nimemweleza kwamba namwamini na kumtegemea kwa mafanikio ya timu yetu,” akasema kocha huyo.
 
 

51.556707-0.11774

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version