Menu
in , , ,

Mourinho, wachezaji wavurunda

Naughty José.

Kocha wa Tottenham Hotspur, Jose Mourinho na baadhi ya wachezaji wake wamekwenda kinyume cha maelekezo ya Serikali ya Uingereza ya kujifungia ndani na kukaa peke peke.

Mourinho aliyekuwa maarufu kwa majina kama The Special One, The Only One na The Happy One, sasa amejikuta akipachikwa jina la ‘The Sorry One’ baada ya kutoka na wachezaji kwenda uwanjani na kufanya mazoezi.

Tayari kocha huyu Mreno aliyepata kuwika na timu kadhaa kama Porto, Chelsea, Real Madrid na Manchester United amekiri kwamba amevurunda kwa kitendo chake hicho wakati huu mgumu wa janga la virusi vya corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu.

Alichukuliwa picha akiwa na mchezaji aliyevunja rekodi ya usajili, Tanguy Ndombele akimfanyisha mazoezi kwenye uwanja jijini hapa. Amesema “matendo yangu hayakuendana na protokali ya serikali.”

Mourinho alikuwa kwenye Uwanja wa Hadley Common na mchezaji huyo, lakini pia wengine -Davinson Sanchez na Ryan Sessegnon walioonekana kwenye mkanda huo wakikimbia kuzunguka uwanja huo. Mlinzi wa Spurs, Serge Aurier naye alikuwa kwenye matukio hayo yaliyokatazwa, na alipandisha picha kwenye mtandao wa Instagram akifanya mbio za pole.

Oh The People’s Tottenham Hotspur! How could you be so reckless?
Oh The People’s Tottenham Hotspur! How could you be so reckless?

Spurs wamesema kwamba tayari wamezungumza na wachezaji kuwaonya na kuwakumbusha haja ya kuheshimu maelekezo ya serikali ya kujikinga na yawezayo kusambaza zaidi virusi hivyo hatari. Askari polisi wa jijini London wamesema kwamba tayari wameshapata taarifa juu ya mkanda wa jamaa hao waliotoka na kufanya yasiyoruhusiwa lakini hawajafikishiwa malalamiko yoyote juu ya hayo.

Mourinho amesema kwamba wamekosea kufanya hayo na kwamba wanaweza tu kukaa au kukutana na wanafamilia wao na si vinginevyo. “Ni muhimu kwamba sote tushiriki katika kufuata maelekezo ya serikali, kuwaunga mkono mashujaa wetu wa kwenye Idara ya Huduma za Afya (NHS) na kuokoa maisha,” yalikuwa maneno yake baada ya kuvuja kwa picha hizo.

Meya wa Jiji la London, Sadiq Khan ameonya akisema kwamba Mourinho na wachezaji wake wanatakiwa kuongoza kwa mifano na si maneno huku matendo yakiwa kinyume. Ligi Kuu ya England (EPL) na Ligi ya Taifa (NFL) zimesitishwa kwa muda usiojulikana kutokana na kusambaa kwa virusi hivyo hatari; watu wakitakiwa kubaki majumbani mwao isipokuwa wenye kazi muhimu kama matabibu na wauzaji wa mahitaji ya lazima.

Khan anasema; “Hofu yangu ni kwamba watu, hasa watoto walio washabiki wa Spurs au hata wa soka kwa ujumla wanaweza kuona picha hizo na kujiuliza ikiwa Mourinho na wachezaji wake ni sawa kutoka na kwenda kucheza, kulikoni wao (watoto) wasifanye hivyo?

“Sioni kulikuwa na ulazima gani kutoka na kwenda pamoja kwenye mazoezi tena wakiwa karibu karibu kabisa na watu ambao huenda wamebeba virusi husika. Hiyo ni kama makusudi tu na moja ya njia za kusambaza virusi hivi.”

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Exit mobile version