*Wakala wa Pogba hotelini kwa Real Madrid
*Liverpool na Depay, Falcao kubaki Man U?
Bosi wa Chelsea, Jose Mourinho anayetarajiwa kusaini mkataba mpya kujifunga Stamford Bridge hadi 2019 anatarajia kufumua kikosi chake.
Mourinho anayedaiwa atavuna pauni milioni 50 kwenye mkataba wake mpya, anapanga kumsajili winga wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann, 24.
Pia, inaelezwa anaungwa mkono na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich ili amsajili mshambuliaji wa Lyon, Alexandre Lacazette, 23, mlinzi wa Real Madrid, Raphael Varane, 22 na golikipa wa Getafe, Vicente Gu.
Wanafuatilia pia kwa karibu hali ya winga Gareth Bale wa Real Madrid na mchezaji wa Barcelona, Pedro, atakayeruhusiwa kuondoka Nou Camp kiangazi hiki. Mipango ni kumruhusu kipa Petr Cech, 32, aondole ambapo kiungo Mbrazili, Oscar jhuenda akauzwa na beki wa pembeni, Filipe Luis anaweza kurudi Atletico Madrid baada ya kukaa Stamford Bridge kwa msimu mmoja tu.
Manchester United huenda wakambakiza mshambuliaji wa Monaco, Radamel Falcao kwa mkopo kwa msimu wa pili ikiwa kipa David De Gea atakubali kusaini mkataba mpya.
Wakala wa wachezaji hao ni raia wa Ureno, Jorge Mendes na inaelezwa hakuna uhakika kwa Falcao kurudi Monaco.
United pia wanataka kumsajili kiungo wa Vitoria Guimaraes, Bernard Mensah, 20, anayefananishwa na Yaya Toure wa Manchester.
Beki wa kushoto wa Man United, Luke Shaw, 19, ameingia kwenye sintofahamu baina ya klabu na Kocha wa Timu ya Taifa ya England, Roy Hodgson.
Hodgson anataka ampange ili acheze mechi dhidi ya Slovenia Juni 7 lakini Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal anamtaka apumzike.
Arsenal wanaandaa ofa kwa beki wa kati wa Monaco, Aymen Abdennour, 25, na mshambuliaji wa Lyon, Nabil Fekir.
Wakala wa kiungo wa Juventus, Paul Pogba, 22, ameonekana akiwa kwenye hoteli waliyofikia timu ya Real Madrid kabla ya mechi yao dhidi ya Juventus nchini Italia.
Manchester City wanapanga kumsajili beki wa pembeni wa Tottenham Hotspur, Danny Rose kwa pauni milioni 15.
Liverpool wapo katika nafasi nzuri kumsajili mchezaji wa PSV Eindhoven ya Uholanzi, Memphis Depay kwa pauni milioni 22
Kipa wa Marseille, Steve Mandanda, 30, yupo tayari kusajiliwa na klabu za Ligi Kuu ya England. Pamekuwapo tetesi kwamba huenda akamrithi Mfaransa mwenzake, Hugo Lloris wa Spurs iwapo atahamia Manchester United.
Man U wamepata pigo baada ya beki wa kulia wa
Southampton na England, Nathaniel Clyne, 24, amesema anataka kubaki Saints.
Everton huenda wakamkosa Aaron Lennon aliye Everton kwa mkopo, kwani Spurs wanataka pauni milioni 29 ili wawauzie mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28.
Timu iliyopanda daraja kwa ajili ya msimu ujao, Bournemouth, wamevunja rekodi kwa kutoa ofa ya pauni milioni tano ili kumpata mshambuliaji wa Sporting Braga, Eder.
Mlinzi wa Liverpool, Martin Skrtel, 30, bado hajakubali kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu aliopewa na klabu hiyo.