Menu
in

Morrison ‘kusepa’ Yanga

yanga

yanga

Kupitia ‘App’ ya timu ya Yanga imetoa sababu za winga wao Benard Morrison kutimuliwa kambini wakati wa kujiandaa na mchezo wa nusu fainali ya kombe la ‘Azam Sports Federation Cup’ dhidi ya Kagera Sugar.

Nidhamu ndio sababu aliyoitoa kocha mkuu wa timu hiyo Luc Aymael kwa Mghana huyo, akieleza kuwa alikuwa anaongea naye mara kwa mara lakini nyota huyo habadiliki hivyo aliamua kumuondoa na kuliacha swala lake kwa uongozi.

Moja ya chapisho la klabu kutoka katika ‘App’ yao linasema kuwa  ‘’Huenda Yanga italazimika kuvunja mkataba wake kwa kigezo cha nyota huyo kurudisha gharama zote ambazo GSM wametumia kumleta nchini,’’.

Limeibua maswali mengi na kuona kwamba ataweza kuondoka ndani ya timu hiyo kama atakidhi matakwa hayo ya kurudisha gharama zote ambazo zinaweza kupelekea kuondoka klabuni hapo.

Maelezo ya kocha wa Yanga Luc Aymael pia yanaashiria kuchoshwa na mwenendo wake.

Eymael amesema suala la nyota huyo ameuachia uongozi wa Yanga kuamua kwani pamoja na kuzungumza nae mara kadhaa, ameendelea kuwa ‘mtukutu’

“Niliamua kumuondoa kambini baada ya kutoridhishwa na tabia yake. Nimezungumza nae mara kadhaa lakini nasikitika amebadilika sana. Huyu sio Morrison niliyemleta hapa, sifahamu amekumbwa na nini”

“Sitaki kulizungumza zaidi suala lake, nimewaachia viongozi wa Yanga kuamua nini cha kufanya,”  alisema Eymael.

Inaelezwa juzi usiku Morrison alijaribu kutoroka kambini kabla ya kudhibitiwa na walinzi wa Yanga ambao alifikia hatua ya kutaka kupigana nao.

Ni dhahiri huyu sio aina ya mchezaji ambaye Yanga wanahitaji kuendelea kuwa nae

Huenda Yanga italazimika kuvunja mkataba wake kwa kigezo cha nyota huyo kurudisha gharama zote ambazo GSM wametumia kumleta nchini.

Kama sivyo anaweza kukaa ‘juu ya mawe’ kwa miaka yote miwili ya mkataba wake kwani hata kama akiamua kuondoka, Yanga itaendelea kushikilia ITC yake na hivyo hawezi kuruhusiwa kuitumikia timu yoyote bila ya ITC hiyo.

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

Leave a Reply

Exit mobile version